Adama Barrow aapishwa kuwa Rais wa Gambia
Adama Barrow, mtu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo.
Alikula kiapo hicho katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi zao.
''Mimi Adama Barrow ,naapa kwamba nitatekeleza wajibu wangu katika afisi ya urais wa taifa la Gambia kwamba nitahifadhi na kutetea katiba'' .
Na katika hotuba yake ya kuapishwa ,aliwaagiza wanachama wote wa jeshi la gambia kusalia katika kambi zao. ''Wale watakaopatikana wakibeba silaha watachukuliwa kuwa waasi'', alionya.
Rais mpya wa Gambia Adama Barrow baada ya kuapishwa |
Wasifu wa rais mpya wa Gambia Adama Barrow
-Adama Barrow alizaliwa mwaka 1965 katika kijiji kimoja karibu na mji wa kibiashara wa Basse Mashariki mwa Gambia.
- Alihamia mjini London miaka ya 2000 ambapo anaripotiwa alifanya kazi kama mlinzi kwenye duka moja, Kaskazini mwa London, akiendelea pia na masomo yake.
- Alirejea nchini Gambia mwaka 2006 ambapo alianzisha kampuni yake ya kuwekeza.
-Barrow mwenye umri wa miaka 51 aliteuliwa kuongoza muungano wa vyama saba vya upinzani kumpinga Rais Yahya Jammeh.
-Amekosoa kutokuwepo kwa miula miwili kwa urais na pia kulaani kufungwa kwa wanasiasa wa upinzani.
-Anaunga mkono uhuru wa mahakama, wa vyombo vya habari na wa vyama vya umma.
Chanzo BBC Swahili
Post a Comment