Halmashauri ya Wilaya ya Monduli yalaumiwa Kuhusu Migogoro ya Ardhi
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota
Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa
ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo.
wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota
Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya.
Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo. |
Na Woinde
Shizza, Arusha
Baadhi
ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo
na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima
baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao
Hayo wamesema jana wakati walipokuwa
wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya
kilichopo ndaniya halmashauri
ya Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa
na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya
300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo
walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao
unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi
wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu
zao .
Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa
jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa
uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo
hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na
kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza wananchi
kulingana na chama ambacho anatokea.
“Tumekuja apa siku nyingi lakini
tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na
chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni
wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi
tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama wa CCM hamna
mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana
na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hayo hayo
kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke
ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii
sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa
sana”alisema Amina Longitoti.
Akiogea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya
Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na
Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama chao hakitakaa
kimya kwa hilo.
Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na
watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika
kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya
kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika
msitu huo kinyume cha sheria.
Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa
na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari
kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi .
“mimi nilipata shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na
sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa
CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha
kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita
vumilia kabisa na kingine
kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu
ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili
pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini
nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu “alisema Sanare
Kwa upande
mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la
Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya
halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio
jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala
hili kwani wananchi hao wanateseka na
hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa
katika viwanja vyao.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni
upepo mchafu unaovuma kupitia.
Hivi karibuni Baraza la madiwani la
Halmashauri ya wilaya ya Monduli, lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya
kijiji hicho kwa madai kuwa waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo
mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.
Post a Comment