Serikali ya TANZANIA kuandaa Sera ya Lugha
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
James Wambura akizungumza na washiriki wa kongamano la Lugha ya Kiswahili
liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar
es Salaam.
.............................
.............................
Na Raymond Mushumbusi
Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza rasmi kuandaa Sera ya Lugha ambayo itatoa muongozo kwa taifa kuhusu masuala yote ya maendeleo ya Lugha nchini ikiwemo Lugha ya Taifa ya Kiswahili.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati akifungua kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Anastazia Wambura amesisitiza kuwa kwa kipindi kirefu sana kumekuwa na uhitaji wa Sera ya Lugha ambayo itasaidia katika ukuaji na matumizi sahihi ya Lugha hasa Lugha ya Taifa ya Kiswahili.
“Kwa hivi sasa rasimu ya awali imeandaliwa na tunaendela kupokea maoni kutoka kwa wadau na kuyachambua” Alisistiza Mhe. Anastazia.
Ameeleza kuwa Sera ya Lugha itasaidia Lugha za Asilia, Lugha za alama , maandishi ya nukta nundu na Lugha za kigeni kuwekewa mkakati wa kuzishughulikia na kuzitumia kwa kukidhi mahitaji ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Shani kitogo ameeleza kuwa mchakato wa kupokea maoni unaendelea na amewaomba wadau wa Lugha hasa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuendelea kutoa maoni yao kwa ajili ya kupata Sera ya Lugha iliyo bora na itakayosaidia katika maendeleo na ukuaji wa Lugha nchini.
“Niwaombe wadau wa Lugha nchini waendelee kuleta maoni yao kwetu ili kuweze kufanikisha kupata Sera ya Lugha kwa Maendeleo ya Taifa Letu” Alisisitiza Bibi Shani.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh ameishukuru Serikali ya waamu ya Tano kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wadau wa Lugha kwa kuanza kuandaa Sera ya Lugha itakayoleta maendeleo katika ukuaji wa Lugha nchini.
“ Niishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa sikivu kwa wananchi na wadau wa maendeleo na tunaahidi kutoa ushirikiano katika uandaaji wa Sera hii ya Lugha”Alisisitiza Bw Byabato.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
James Wambura akisalimia na Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo
vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh alipowasilia katika Chuo
cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere katika kongamano la Lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
James Wambura akisalimia na Waziri zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt
Mohamed Seif Khatib wakati alipowasili katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu
Nyerere kufungua kongamano la Lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
James Wambura akiweka saini katika kitabu cha wageni mara alipowasilia katika
Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere katika kongamano la la Lugha ya
Kiswahili.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
James Wambura (katikati) akielekea katika Ukumbi wa Utamaduni katika Chuo cha
KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere kufungua kongamano la Lugha ya Kiswahili. kulia
ni Naibu Mkuu wa Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere( Mipango Fedha na
Utawala) Dkt. Magreth Shawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa
Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh.
Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Shani kitogo akiimba ushairi katika ufunguzi wa kongamano la la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
James Wambura akipokea Risala kutoka kwa Bw. Sarungi Innocent aliyesoma risala
kwa niaba ya Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki
(CHAWAKAMA) wakati wa ufunguzi wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika
katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es
Salaam.
Mlezi wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika
Mashariki (CHAWAKAMA) na Waziri zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt
Mohamed Seif Khatib akitoa mada mbalimbali kuhusu Lugha ya Kiswahili katika
kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya
Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Riwaya Bw. Shafi Adam Shafi
akitoa mada mbalimbali kuhusu Lugha ya Kiswahili katika kongamano la Lugha ya
Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni
Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment