Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akisalimia
wanachama wa Chama cha
Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa
mwaka Uliofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 19
Januari, 2017.
...............................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameshauri uongozi wa Chama cha Akiba na
Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu (Makamu Saccos) kuwa na ubunifu katika
utendaji ili kuleta manufaa zaidi kwa wanachama wake.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka
wa Wanachama wa Chama hicho uliofanyika Januari 19, 2017 mkoani Dodoma.
Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwepo
na mikakati madhubuti ya kubuni miradi itakayowezesha chama kuwa na vyanzo
vyake vya mapato na kuwa na mikakati ya kuongeza wanachama wapya kwa kuzingatia
umuhimu wa chama hicho.
“Ni muhimu kuwa na mikakati madhubuti ya kubuni
miradi, kuongeza wanachama pamoja na kuwa na vitu vya kiupekee na vya kiufanisi
vitakavyokisaidia chama kuwa imara katika utendaji wake”, alisema
Waziri Mhagama.
|
Post a Comment