Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yatakiwa Kumnyima tenda Mkandarasi ARRAY
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji
Mtaturu akipoke taarifa ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya sekondari Wembere.
..............................................................................................
KATIKA moja ya mikakati ya serikali
ya awamu ya tano chini ya rais dokta John Magufuli ni kuhakikisha kunakuwepo
mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia ambapo katika kusimamia hilo mkuu
wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amefanya ziara ya kukagua miradi
iliyopo katika mpango wa serikali wa kuwezesha shule za sekondari
nchini(SEDEP).
Katika ziara hiyo Mtaturu amekagua
ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya sekondari ya
Minyughe,Wembere na Msungua na kutoa agizo kwa mkurugenzi la kuvunja mkataba wa
mkandarasi ARRAY TECH SERVICES LTD.
Aidha amepiga marufuku mkandarasi
huyo kupewa kazi tena katika wilaya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na mkandarasi
huyo kwenda kinyume na mkataba ikiwemo kujenga chini ya kiwango.
“Mkandarasi huyu alipewa kazi ya
kujenga madarasa mawili katika sekondari ya Iseke na matundu ya vyoo 10 katika
shule ya Minyughe lakini ameenda kinyume cha mkataba.,”alisema Mtaturu.
Kutokana na hilo amewasisitiza
watendaji kuepuka kutoa tenda kwa mkandarasi yoyote bila ya kujua
historia yao ya kazi.
Ujenzi mwingine uliopo ni wa nyumba
za walimu katika shule ya sekondari ya Minyughe na Wembere ambapo
kukamilika kwake zitasaidia kupunguza tatizo la makazi kwa walimu na
hivyo kuongeza ari ya ufundishaji na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Mbali na kukagua ujenzi wa madarasa
pia Mtaturu amekagua ujenzi wa daraja kubwa la Minyughe linalojengwa na
mkandarasi KINGS BUILDERS AND GENERAL SERVISEC LTD kwa thamani ya shilingi
milioni 924.6 linalotarajiwa kukabidhiwa mwenzi machi mwaka huu.
Kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa
kiungo muhimu kwa wananchi wa kata za Sepuka,Irisya,Makilawa,Minyughe,Puma na
ihanja.
Mtaturu amesema kwa sasa wananchi
wanazunguka umbali wa kilomita 80 kwenda makao makuu ya wilaya lakini
kukamilika kwa daraja hilo kutawafanya wananchi hao kutumia chini ya kilomita
40 hatua ambayo itaongezea uchumi kwa wakulima na kuboresha huduma za kijamii
kwa wananchi kama ilivyoanishwa katika Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
ya mwaka 2015.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji
Mtaturu akikagua ujenzi wa daraja kubwa la Minyughe linalojengwa kwa thamani ya
shilingi milioni 924.6 na kutajwa kuwa kiungo muhimu kwa wananchi wa kata za
Sepuka, Irisya, Makilawa, Minyughe, Puma na Ihanja baada ya kukamilika kwake.
Mafundi wa kutoka kampuni ya ujenzi
ya Kings Builders& General Services LTD wakiendelea na ujenzi wa daraja
kubwa la Minyughe lililopo wilayani Ikungi linalotarajiwa kukabidhiwa machi Mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji
Mtaturu akiwa ameambatana Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Wembere katika
ukaguzi wa ujenzi wa matundu ya choo kwenye shule ya sekondari Wembere.
Post a Comment