Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza
wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro kabla ya kufunga mafunzo ya jeshi Usu yaliyofanyika jana katika
kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi.
.................................
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, amesema
hatamvumilia mtumishi yeyote atayejihusisha
na vitendo vya rushwa kuwa ni lazima ataondolewa mara moja ili asiendelee kuchafua taswira ya Wizara.
Alitoa
rai hiyo jana wakati akifunga mafunzo ya
jeshi Usu kwa wahifadhi wa
wanyamapori 103 kutoka Mamlaka ya
Hifadhi Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori ( TAWA)
na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA).
Alisema
Wizara kwa sasa inabadili mfumo wa kiraia na kuendesha kwa mfumo wa kijeshi hivyo mtumishi yeyote
asiyejihusisha na vitendo viovu vya namna yeyote Yule hatasalimika.
Wakati
huo huo , Maj. Gen. Gaudence Milanzi alifungua
mafunzo ya ukakamavu kwa maafisa wanyamapori wa daraja la pili kutoka TAWA yatakayochukua muda wa wiki tano lengo likiwa ni kuwandaa watumishi wa taasisi
hiyo katika kuboresha mbinu za kupambana na majangili.
Akizungumza jana na wahitimu hao kabla ya
kufunga mafunzo hayo katika kituo cha
Mafunzo cha Mlele mkoani Katavi ,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Maj. Gen. Milanzi aliwataka wahifadhi
hao wakaoneshe kile walichojifunza kwa kwa kujenga mahusiano mazuri na wanavijiji
wanaozunguka hifadhi nchini baadala ya
kujenga uadui.
Aliwasihi
wahitimu hao kutumia silaha kwa weledi pale inapobidi hasa inapohitajika
kunusuru maisha ya watu na sio kuua.
Aidha,
Milanzi aliwaagiza wakuu na viongozi wa taasisi zote zilizo
chini ya Wizara wahakikishe wanashiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa
Wizara inatoka kwenye mfumo wa kiraia na kuelekea kwenye mfumo wa kijeshi katika utendaji wa shughuli
za uhifadhi nchini.
Akitoa
maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii,
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, David Kanyatta aliwataka wahifadhi
waliopewa mafunzo hayo wakajitume kwa kufanya kazi kwa bidii katika vituo vyao vya kazi ili kuonesha tija
kwa taifa katika uhifadhi.
Kabla
ya kuwahutubia wahitimu hao, Katibu Mkuu Milanzia alioneshwa mbinu mbalimbali
kwa vitendo walizojifunza katika kupambana majangili ambao wamekuwa wakitumia
silaha nzito wakati wakifanya ujangili.
|
Post a Comment