Watanzania Washauriwa Kutumia Fursa ya Kuwekeza Mkoani SIMIYU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisisitiza jambo wakati
akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.
......................
Na Mathias Canal, Simiyu
Wafanyabiashara na wadau wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji wa biashara hususani katika kuwekeza kwenye viwanda kwani mipango mingi inayopangwa na serikali inatoa fursa zaidi kwa wawekezaji wa ndani ya nchi jambo ambalo litaifanya Tanzania kuondokana na umasikini kutokana na fursa zilizopo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu lililofanyika katika Ukumbi wa Parokia ya Mtakatifu John lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Rc Mtaka amesema kuwa Katika kuchochea na kuleta maendeleo kwa wananchi katika Mkoa wa Simiyu uongozi wa Mkoa huo una dhamira ya dhati kuwafanya wananchi wake kuingia katika ramani ya Mkoa unaotumainiwa nchini.
Wadau wengine walioshiriki katika Jukwaa hilo la Biashara ni pamoja na TIB Development Bank, National Microfinance Bank (NMB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na TIB Development Bank Ltd.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati), Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel
(kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya
serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakisikiliza
maelezo mbalimbali katika Kongamano hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel
akisisitiza umuhimu wa Viwanda nchini Tanzanai.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate
Bank Ltd Bi Theresia Soka (kulia) akiwa na Zacharia Kicharo Meneja wa TIB Development
Bank Ltd Lake Zone wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi
wa Kongamano la Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg Jumanne Sagin
akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
kuzungumza na wafanyabiashara na wawekezaji waliojitokeza katika kongamano la
uwekezaji.
Kutoka Kulia ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa
Viwanda Mkoa wa Simiyu, Peter Bahini Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza
Kusini (SNC) na Emmanuely Lupembe Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini
(SNC wakifatilia kwa makini kongamano la uwekezaji Mkoani Simiyu.
Post a Comment