Baada ya Miaka 53 Wananchi wa Mtaa wa IGUNGANDEMBWE wapata Maji Safi na Salama
Mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
................................
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.
Wakizungumza na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.
“Angalia maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.
Wananchi wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia.
Mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye aliyechimba kisima hicho.
Mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo.
Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima.
Post a Comment