Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Millya (wa nne
kulia) na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe.
Dunstan Kitandula, Mbunge wa Mkinga (CCM), (wa pili kulia),
Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) (wa Tatu kulia) na wakipata maelezo
kuhusu biashara ya Tanzanite ndani ya duka la The Tanzanite Experience jijini Arusha. Anayetoa maelezo ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hasnain Sajan. Wa kwanza kushoto ni Kamishna
Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Adam Juma.
..........................
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa
Simanjiro, Mhe.James Millya, wametembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha
ili kujionea shughuli za biashara na uongezaji thamani wa madini hayo
zinavyofanyika.
Ziara
hiyo ni moja ya majukumu waliyopanga kuyafanya jijini Arusha, jukumu kuu likiwa
ni kushuhudia jinsi Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite unavyofanyika
katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha.
Moja
ya duka lililotembelewa na Wabunge hao ni The
Tanzanite Experience ambalo hujishughulisha na kukata Tanzanite ili kuiweka
katika maumbo mbalimbali na kuing’arisha.
Duka la The
Tanzanite Experience pia hutoa elimu bure kwa wanafunzi na wageni
mbalimbali kuhusu madini ya Tanzanite ikiwemo historia yake.
Ndani ya
duka hilo pia kumejengwa mgodi wa mfano wa
Tanzanite ambao hutumika kutoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu shughuli za
uchimbaji wa Tanzanite.
Baadhi ya Wajumbe waliofanya ziara hiyo ni pamoja
na Mhe. John
Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa
Bububu (CCM) na Mhe. Dunstan Kitandula
Mbunge wa Mkinga (CCM).
|
Post a Comment