Mwakilishi Mkazi wa UNDP aongoza Zoezi la Upandaji Miti Mlima Kilimanjaro
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Maruwa wilaya ya Moshi vijijini mara baada ya kuwasili kwa ajili ya shughuli ya kuotesha miti 120 katika eneo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na wageni wengine wakitizama mnara wa kumbukumbu uliowekwa katika eneo hilo baada ya kufanyika kwa shughuli za uoteshaji miti 1510 mwaka 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi
Celestine Mushi akiotesha miche ya miti katika eneo hilo.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiotesha miti katika eneo hilo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Post a Comment