Takwimu Zinazoonesha hali ya Uzazi Salama Nchini Tanzania
Inakadiriwa kuwa, mimba 405,000 zilitolewa ndani ya mwaka
2013 nchini Tanzania. Idadi hii ni kiwango cha utoaji wa mimba 36 kwa kila
wanawake 1,000 wenye umri kati ya miaka 15-49 na uwiano wa utoaji mimba 21 kwa
kila watoto 100 wanaozaliwa wakiwa hai.
•Nchini Tanzania, viwango vya utoaji mimba hutofautiana
sana kwa ukanda, kutoka 11 kwa wanawake 1,000 kwa Zanzibar hadi 47 kwa Nyanda
za Juu Kusini na 51 kwa Kanda ya Ziwa. Ukanda wa Ziwa na Nyanda za Juu Kusini
huwa na viwango vya juu vya matibabu kwa matatizo yatokanayo na utoaji mimba
pia.
•Mwaka 2013, katika
nchi nzima, 15% ya mimba zilitolewa, 52% katika uzazi uliokusudiwa, 18% katika
uzazi usiokusudiwa na 15% katika mimba zilizoharibika. Mgawanyo huu
hutofautiana kwa maeneo kwa mfano, uwiano wa mimba zilizotolewa ni kati ya 6%
kwa Zanzibar hadi 18% kwa Nyanda za Juu Kusini.
(Chanzo: guttmacher.org)
Kupunguza utoaji mimba usio salama na vifo vya wajawazito na majeraha yanayohusishwa na utoaji mimba, utahitaji kupanua upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango ili kuzuia mimba zisizotarajiwa, na kupanua upatikanaji wa huduma za baada ya kuharibika kwa mimba.
Vituo vya afya katika ngazi zote lazima viwe na dawa muhimu za kutosha, vifaa vya kutolea huduma za msingi za baada ya kuharibika kwa mimba, na watoa huduma wa kawaida wanapaswa wapewe mafunzo ya kutoa huduma hizo.
Utata kuhusu sheria ya utoaji mimba ya Tanzania unatakiwa ufafanuliwe ili kusaidia kuunga mkono taratibu salama na kisheria zitumike kikamilifu, na kuhakikisha kuwa wanawake hawana sababu ya kuamua kutumia njia zisizo salama kutoa mimba zao.
Post a Comment