Wanachama wa PSPF Sasa Kupata Mikopo Kupitia Benki ya CRDB
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
Na Khalfan Said
WANACHAMA
wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya
CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa
mpango huo baina ya taasisi hizo mbili jana jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo
, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw
Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa wanachama ulianza
tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za kifedha.
Alisema
kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana
kushirikiana katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.
Mikopo
hiyo ni pamoja na mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia
maisha( startup life loan scheme) na mkopo wa viwanja (Nipo site na PSPF)
Alisema
kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu , mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya
kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni stashahada, shahada, shahada ya uzamili na
hata mafunzo ya ufundi.
Kwa
upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema mwanachama aliyepata ajira kwa mara
ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu
na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa
kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya
ajira.
Kuhusu
mkopo wa viwanja kwa wanachama, alisema kuwa
huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya
makazi ambavyo vinapataikana maeneo
mbali mbali ya nchi.
“Lengo kubwa hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF
kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika
makazi holela, ambayo yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi
yaliyopangiliwa”,alisema.
Alifafanua
kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania
anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika
masomo kupitia mkopo wa elimu , ndoto
yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
Hadi
kufikia tarehe 17 Mwezi huu idadi ya wanachama walionufaika na mikopo hiyo na idadi kwenye mabano ni Elimu (1,432)),
mkopo wa kuanzia maisha ( 847), mkopo wa viwanja (58).
k Charles Kimei, alisema
azma yao ni kuhakikisha kuwa ushirikiano na wadau wanamkomboa kiuchumi
mwananchi hususan mwenye kipato cha
chini kwa kumpatia mkopo wenye riba ya asilimia 14 tu kwa mwaka.
Kuhusu marejesho alisema ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Kuhusu marejesho alisema ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Ushirikiano
wetu na PSPF bado una muendeleo ulio
mpana kwani kwa pamoja tunadhamiria hapo baadae kuingiza sokono mikopo kwa
ajili ya wastaafu ‘pensioners’.
Alisema
mpango huu wa utoaji wa mikopo kw wastaafu una lengo la kuleta faraja na
kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbali mbali ya kimaisha ikiwamo
kulipia gharama za matibabu, ada za shule za watoto au wajukuaa na kuendesha biashara ndogo ndogo
zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya kila siku.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo.
Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akitoa hotuba ya ukaribisho.
Viongozi wa juu wa PSPF, wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya maafisa wa CRDB waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mipangona Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akitoa neno la shukrani mwishoni mwa hafla hiyo.
Anna Lukando wa kampuni ya Ardhi Plan Limited, yenye ushirikiano na PSPF, akizungumzia jinsi wanachamawa Mfuko huo wanavyoweza kufaidika naupatikanajiwa viwanja vilivyopimwa kisheria.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango huo, mfanyakazi wa CRDB, Bi. Fausta Urassa.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bw.Alfred Kessy.
Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bi. Flora Munisi. |
Uzinduzi rasmi ukifanyika...
Post a Comment