Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari, (hawapo pichani), mara baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la tatu la
Abiria (TB III), jijini Dar es Salaam.
............................
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameteua timu mpya ya wataalamu saba
kwa ajili ya kusimamia mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal
III), katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Hatua hiyo
imefikiwa kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais John Magufuli alilolitoa jana
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza uwanjani hapo kujionea maendeleo yaliyofikiwa katika mradi
huo.
Timu hiyo inaongozwa
na Eng. Julius Ndyamukama inaundwa na Eng, Godson Ngomuo, Eng. Humphrey Kanyenye,
Eng. Abednego Lyanga, Eng. Mbila Mdemu na Eng. Rehema Myeya.
“Naamini timu
hii ina wataalamu mahiri, hivyo itasimamia ujenzi huu kukamilika kwa wakati na
kwa kuzingatia thamani ya fedha (value for money”, amesema Waziri Mbarawa.
Profesa Mbarawa
amemhakikishia mkandarasi wa kampuni ya BAM kutoka uholanzi inayojenga jengo
hilo kuwa Serikali itamlipa mkandarasi huyo katika kipindi cha wiki mbili
kutoka sasa.
Aidha, ameitaka
timu hiyo kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika mwezi Desemba mwaka huu
kama ilivyopangwa.
|
Post a Comment