Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata
taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kutoka kwa Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoani humo, Bi. Zitta Majinge
(kulia), mara baada ya kuwasili leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw.
Evod Mmanda.
..............................
Serikali
imesema ina mpango wa kukarabati uwanja wa ndege wa Mtwara
ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua uwanjani
hapo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo.
Akizungumza
mara baada ya kukagua uwanja huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa ukarabati huo utahusisha njia ya kuruka na
kutua ndege, maeneo ya maegesho pamoja na barabara yenye urefu wa km 1.5
inayoingia katika uwanja huo.
"Tunategemea
mwisho wa mwezi huu kutangaza zabuni ya ukarabati wa uwanja huu, matumaini yetu
tutampata mkandarasi mzuri kwa ajili ya kazi hii", amesema Waziri Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa amefafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa inajenga uzio katika uwanja huo ili kuhakikisha
usalama wa uhakika uwanjani hapo.
|
Post a Comment