Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na
Mwakilishi wa Shirika la Chakula
na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998
ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani
miaka 19 hadi hivi sasa. ................................
Serikali ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa
(FAO) wameisaini makubaliano ya kupitia
upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka
1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa
takribani miaka 19 hadi hivi sasa.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi amesema mpango huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni
280 ambazo zimetolewa na FAO kwa ajili
ya kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya Misitu ya
Taifa ili iweze kufikia hadhi ya
kimataifa.
Amesema hatua hiyo imekuja Kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka
1998 inayotumika hadi hivi sasa kupitwa na wakati yakiwemo mabadiliko ya Kiuchumi, Kuongezeka kwa idadi
ya watu pamoja na Mabadiliko ya tabia ya nchi.
Maj. Gen. Gaudence ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la ufyekaji misitu na hivyo kumechangia kupunguza uoto wa asili kutoka hekta milioni 55.9 kwa mwaka 1990 hadi kufikia hekta milioni 46 kwa sasa lakini Sera ya Misitu ni ile ile.
‘’ Sera ya Taifa ya Misitu ilishafanyiwa mapitio kuanzia
mwaka 2009, Lakini kutokana na Sera hii kukaa kwa muda wa takribani Miaka 9
hadi hivi sasa tumegundua kuwa baadhi ya
wadau wengi hawakupata nafasi ya kutoa mawazo yao. Hata wale waliotoa mawazo
yao mengi yameshapitwa na wakati.’’ Alisema Maj. Gen. Milanzi.
Naye Mwakilishi Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero amesema
kuwa Mradi huo utasaidia wananchi wengi kushiriki na kutoa mawazo mengi
kuhusiana na Sera ya Misitu ikiwa pamoja na
kuwajengea uwezo watumishi kuweza kukusanya taarifa nyingi ili ziwezeshe kuboresha sera kupitia tafiti.
Aidha,Kafeero amesema kutokana na mabadiliko hayo FAO itasaidia katika kuhuisha sera mpya ambayo itatoa majibu kwa changamoto
zinazoikabili nchi hivi sasa na kukidhi mikataba ya kimaifa kama vile
mabadiliko ya tabia ya nchi.
|
Post a Comment