Header Ads

Mama SAMIA SULUHU aunga Mkono Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kukabidhi matembezi ya Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, Makao Makuu ya nchi Dodoma.



Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi mapema leo asubuhi mjini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.Pichani kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.


Mbali ya Makamu wa Rais kuunga mkono tukio hilo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye ,Naibu Spika wa Bunge,Tulia Ackson,Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba,Naibu waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla na wengineo sambamba na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma.


Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza mazoezi ya kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.



Wananchi kutoka vitongoji mbalimbali vya mji wa Dodoma wakishiriki mazoezi mapema leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.

No comments

Powered by Blogger.