Mkufunzi
Msaidizi katika Kituo cha Jemolojia Arusha, (TGC), Lilian Petro (wa kwanza
kulia) akionyesha madini ya vito yaliyong’arishwa na wanafunzi wanaopata
mafunzo katika Kituo hicho kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini. Wa
Pili kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito
(TANSORT), Archard Kalugendo, wa Pili kushoto ni Mhe. Catherine Magige, Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) na wa kwanza kushoto ni Beatrice Lupi, Mhasibu Mkuu kutoka
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
.............................
Imeelezwa
kuwa jumla ya wanawake 47 wamehitimu
mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito yanayotolewa na Kituo cha
Jemolojia jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Hayo
yalisemwa jijini Arusha na Kaimu Mratibu wa Kituo hicho, Erick Mpesa wakati wa
Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite unaofanyika jijini Arusha
katika Kituo hicho.
Mpesa
alisema kuwa mafunzo hayo yalianza kutolewa mwaka 2014 ambapo katika Awamu ya
kwanza wanafunzi 15 walihitimu, Awamu ya Pili walihitimu wanafunzi 14 na Awamu ya Tatu walihitimu
wanafunzi 18.
“Mafunzo
haya hutolewa kwa muda wa miezi Saba ambapo
Wanafunzi hawa ambao huwa na umri wa
chini ya miaka 30 wanafadhiliwa na Mfuko wa Kuwaendeleza Wanawake chini ya
Kamati ya Maonesho ya Vito ya Arusha (AGF) na Wizara ya Nishati na Madini,”
alisema Mpesa.
Mratibu
wa TGC aliongeza kuwa Kituo hicho pia
kinaendesha shughuli za uchongaji wa
mawe ya miamba kwa kutengeneza vinyago vyenye maumbo mbalimbali kama ya
wanyama, ndege, samaki na vitu mbalimbali vya urembo.
|
Post a Comment