Watu 50 Wamefariki Kwenye Mafuriko Nchini ETHIOPIA
Takriban watu 50 wamefariki kufautia
mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya
maeneo Ethiopia.
Taifa hilo la upembe wa Afrika
linakabiliwana ukame mbaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka 50 huku watu zaidi
ya milioni 10 wakiwa wanahitaji msaada wa dharura wa kibinaadamu.
Ukame huo umezidhishwa kuwa mbaya
kutokana mvua ya El Nino inayoaathiri baadhi ya mataifa Afrika mashariki na
kusini.
Maafisa wa serikali katika wilaya
iliopo kusini mwa Ethiopia Wolaita wamekiambia kituo cha televisheni ya
serikali kuwa watu 41 waliuawa Jumatatu katika maporomoko ya ardhi yaliotokana
na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini.
Post a Comment