Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akiwakabidhi zawadi ya kikombe washindi wa
pili wa Mbio za Magari za Alliance Auto MMSC Rally Dharam Pandya (katikati) na
Manmeet Singh kutoka Timu ya Puma Energy.
.................
“Natoa
wito kwa wadau wa mchezo huu ili muweze kufanikiwa zaidi anzisheni Chama cha
Kitaifa kitakacho kuwa daraja la kushughulikia masuala yote yahusuyo mcheo huu
kwa matiki hiyohiyo nawakaribisha Wizarani ofisi zipo wazi” Alisema Nkenyenge.
Aidha
ametoa rai kwa wadau wa mchezo huo kuangalia namna watakavyoweza kuufikisha
mchezo huo katika ngazi za chini zaidi ili vijana wengi waweze kushiriki.
Naye
mratibu wa mashindano hayo kutoka Mzizima Motor Sports Club Bi. Hidaya Kamaga
ameishukuru Serikali kwa kukubali kushiriki mashindano haya kama mgeni rasmi.
Kamaga
alisema kuwa amesikia wito wa Serikali na wako tayari kukaa pamoja ili wapate
muongozo wa namna ya kuanzisha Chama cha Mchezo wa Mbio za Magari hapa nchi.
Kwa
upande wake mshindi wa kwanza wa
mashindano hayo Jamil Khan amemeshukuru kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo
pamoja na kukumbana na changamoto ya kuzimikiwa na gari kabla ya kufika kituo
cha mwisho hali iliyowalazimu kuendelea na mashindano kwa kusukuma gari hadi
mwisho wa kituo.
Khan
ameongeza kuwa ushindi aliopata umempa faraja na kuahidi kuendelea kuhamasisha
jamii inayomzunguka kujifunza mchezo wa mbio za magari kwani ukiuelewa ni kama
michezo mingine.
Ameongeza
kuwa mchezo huo umeendelea kupata mashabiki hivyo ni dalili njema kuwa mchezo
huu umeanza kukua hapa nchi.
Mashindano
ya mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally 2016 mzunguko wa Tatu
yamezaminiwa yameratibiwa na Klabu ya
Mzizima Motors ya jijini Dar es Salaam na kufanyika wilayani Bagamoyo.
|
Post a Comment