Rais MAGUFULI afanya Uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla ya Uteuzi
huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).
Bw. Mdemu
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.
Kabla ya uteuzi
huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu
cha Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza
kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
23 Mei,
2016
Post a Comment