Mkongwe wa Muziki wa Dansi ZAHIR ALLY ZORRO ashauri Muziki huo Ufufuliwe Jijini MWANZA
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini Tanzania, Zahir Ally Zorro (Kushoto) akizungumza na George Binagi @BMG (Kulia).
............
Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini, Zahir Ally Zorro, amewahimiza wadau wa muziki wa dansi Mkoani Mwanza, kuwaunganisha wanamuziki wa muziki huo ili kuurudisha kwenye chati kama zamani.
Alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza na BMG, ambapo alisema muziki wa dansi nchini umepotea sokoni hivyo jitihada zote zinafanyika ili kuurudisha katika soko, akitolea mfano Mkoani Mwanza ambapo kuna uhaba wa band za muziki wa dansi.
"Muziki wa dansi upo na tunajitahidi kuurudisha katika soko. Mwanza kuna vijana wengi wanafanya muziki wa dansi, wanaposhindwa kusikilizwa na media inauma sana hivyo ni vyema wakaunganishwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya muziki wa Mwanza". Alisema Zorro.
Mbali na hayo, Zorro ambae alianza muziki tangu mwaka 1968, yuko Jijini Mwanza kikazi ambapo leo jumamosi May 14,2016 atakuwa na show kali ndani ya Kilimanjaro Club iliyopo Nyegezi, atakapokuwa akinyukana na wenyeji wake Twiga Band.
Picha na Iman Hezron
Post a Comment