Manchester United yashinda Kombe la FA
Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezewa uwanja wa Wembley.
Ni mara yao ya kwanza kushinda kikombe hicho tangu 2004.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata na Jesse Lingard.
Bao la kufutia machozi la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon.
Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofana kwa klabu hiyo.
Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.
"Ni muhimu sana kushindia klabu kikombe hiki, kwaa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya hivyo," amesema.
Post a Comment