CCM: HAKUNA MGOGORO WA JAKAYA KIKWETE KUKABIDHI KIJITI CHA UENYEKITI KWA Dkt JOHN MAGUFULI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna mgogoro uiopo wa kukabidhiana kijiti cha Uenyekiti ndani ya chama hicho na kuonya vyombo vya habari kuacha kupotosha umma.
"Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhiana kijiti cha Ueneyekiti katika CCM na wala hautakuwepo", amesema, Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo.
Katika taarifa hiyo, Sendeka amesema, baadhi ya vyomo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekoti wa sasa wa CCM Dk. Jakaya Kikwete kukabidhi kiiti cha uongozi wa CCM kwa Rais Dk. John Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya CCM.
"Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti. Hbari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dk. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa isiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu kwa sababu ya kukailisha maandalizi ya ajenda hizo", alisisitiza Sendeka.
Sendeka alisema, dhamira ya CCM kupanga kufanya Mkutano Mkuu Maalum Mwezi Juni 2016, ipo pale pale isipokuwa kilichoelezwa kwenye kikao ni kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo na kwamba mpango wa kutafuta fedha ukikamilika tarehe ya mkutano huo Mkuu Maalum itatangazwa.
Alisema, CCM inawataka wanachama wake wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu aliosema kuwa ni wenye nia mbaya na CCM. "Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila mafanikio", alisema Sendeka.
"Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa na hakukuwa na sababu za kulitaja", alisema Sendeka na kuongeza;
"Aidha tunakanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwnyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi ufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa wabunge wa CCM hayana msingi wowote".
Sendeka alisema, Kamati Kuu iliteua wabunge wanne kugombea na kuwaacha wabunge wa CCM kuamua na kwamba kuhusisha viongozi na hasa kuzua kuwepo kutkuelewana ni jambo la kusikitisha na kwamba ni taarifa yenye uongo, yenye nia ovu kwa CCM na viongozi wake.
"Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukeli waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza katika jamii, badala yake waheshimu maadili ya kazi yao", alisema Sendeka.

Post a Comment