Watakaozidisha Nauli Kwenye Mabasi ya Abiria Kukiona Jijini TANGA
Mamlaka ya Usimamizi wa vyombo vya
usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoani Tanga kwa kushirikiana
na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wameanza operesheni
maalumu kwa madereva wanaozidisha abiria na nauli kwenye mabasi
yanayotoka mikoa mbalimbali ikiwemo kanda ya kaskazini.
Hatua inafuatia idadi kubwa ya abiria ambao wanatoka mikoa hiyo kurejea
mkoani Tanga na maeneo mengine hivyo baadhi ya mabasi wanapandisha nauli
kiholea na kuzidisha abiria.
Hayo yalisemwa na Ofisa Sumatra Mkoani Tanga, Dkt Walukani
Luhamba (Pichani Juu) wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema
waliamua operesheni hiyo ili kuweza kudhibiti
masuala hayo ambayo yamekuwa yakiwapa wakati mgumu wananchi wanaotumia
vyombo hivyo kwa ajili ya matumizi yao.
Operesheni hiyo inafanyika kwenye maeneo ya Mombo,Korogwe, Mkata na
Segera ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili
kuweza kuikomesha kwa madereva wenye tabia kama hiyo.
Dkt Walukani alisema katika kuhakikisha wanazibiti operesheni hiyo hivi
sasa wanamshikilia dereva wa basi la Hood Issa Kayela (30) linalofanya
safari zake kutoka mkoani Arusha kuelekea Mbeya anashikiliwa na Jeshi la
Polisi katika kituo cha Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kosa la
kuzidisha abiria zaidi ya idadi aliyotakiwa kubeba.
Alilitaja basi hilo lilikuwa na namba za usajili T.779 AVL Scania aina
ya Torino lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea Mbeya ambapo baada
ya kumkamata walimpelekwa mahakamani na baada ya kufika huko akukosa
dhamana amerudishwa mahabusu na baade ya wiki mbili anatarajiwa
kupandishwa kizimbani.
Akizungumza hatua inayofuata,Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva
huyo kukaa kwenye kituo hicho kutokana na kukosa dhamana atafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana
na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.
“Ukiangalia basi hilo la hood lilikuwa linapaswa kupakia abiria 51
lakini lilipokamatwa eneo la mkata wilayani Handeni lilikuwa na abiri
80 jambo ambalo ni hatari sana “Alisema.
“Kutokana na hali hiyo dereva wa basi hilo alipelekwa mahakamani na
alikosa dhamani na hivi sasa anashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Mkata
kwa ajili ya kufikishwa mahakamani na ikithibitisha ana kosa basi
atalazimika kwenda Jela mwaka mmoja au miwili hii itakuwa fundisho kwa
madereva wengine wenye tabia kama hii “Alisema.
Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo alikaa kwenye kituo hicho
baada ya kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra
atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.
Naye kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani
Mkoani
Tanga, Nassoro Sisiwayah alisema operesheni hiyo itakuwa endelevu kwa
kufanyika kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ikiwemo Mombo, Korogwe,
Mkata na Segera lengo kubwa kuhakikisha sheria za usafirishaji
zinafuatwa.
Alisema katika operesheni hiyo wanazibiti nauli kwenye mabasi y mikoani
ambayo hivi sasa kwa asilimia kubwa watu wengi wanarudi kutoka mikoa ya
kaskazini ambapo ulanguzi wa nauli umekuwa ukitumika.
Post a Comment