Hii Hapa Taarifa ya Utoaji Ruzuku Kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini Januari 17, 2017
TAARIFA
KWA UMMA
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na
Madini, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) itatoa Ruzuku ya jumla ya Shilingi Bilioni 7.481 kwa Wachimbaji
Madini Wadogo 59 ambapo kiwango cha
juu cha Ruzuku kwa Kikundi/Mtu binafsi ni Shilingi Milioni 210.
Hafla ya utoaji wa Ruzuku
hiyo itafanyika siku ya Jumanne, tarehe
17 Januari 2017, Mjini Mpanda mkoani
Katavi, Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
M. Majaliwa (Mb.).
Fedha za Ruzuku kwa kila Mnufaika, zitatumika
kununua vifaa vya kuchimbia au kuchenjulia madini ambapo kabla ya kukabidhiwa
vifaa hivyo, wanufaika hao watapata mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya ruzuku
yatakayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 16 Januari, 2017 Mjini
Mpanda.
Miradi
59 itakayopata ruzuku hiyo, ndiyo iliyoshinda kati ya miradi 592 ya uchimbaji
madini mdogo iliyokuwa kwenye ushindani.. Waombaji wengine ambao maombi yao
hayakushinda watajulishwa kwa Barua.
Wizara
ya Nishati na Madini ilianza mchujo wa kuwapata Washindi tangu Mwezi Julai 2016,
kwa kuwashirikisha Viongozi wa Wachimbaji Madini Wadogo wa mikoani (REMA’s),Viongozi wa Kitaifa (FEMATA) pamoja na Viongozi wa Wachimbaji
Madini Wanawake (TAWOMA).
Majina
ya wanufaika wa Ruzuku awamu ya tatu pia
yanapatikana kwenye Tovuti ya Wizara: www.mem.go.tz
pamoja na Ofisi Za Madini Za Kanda.
Imetolewa
na,
Prof. Justin W. Ntalikwa
KATIBU MKUU
Post a Comment