Chama cha Soka Mkoa wa Arusha ( ARFA ) chapata Viongozi Wapya
Mwenyekiti mpya wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha
(ARFA) Peter Temu.
...................................
...................................
Na
Woinde Shizza,Arusha
Chama
cha soka Mkoa wa Arusha (ARFA) kimefanikiwa kupata uongozi mpya baada ya
uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Monduli
ambao watakaa madarakani kwa miaka minne.
Katika
uchaguzi huo uliokuwa unawaniwa nafasi kumi, ulionekana mgumu kwa nafasi mbili
pekee ile ya Mwenyekiti pamoja na nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu
wa TFFambapo wagombea walikua wawili wawili.
Waliofanikiwa
kupita katika uchaguzi huo kwa nafasi ya mwenyekiti ni Peter Temu aliyemshinda
Omary Walii kwa kura 13 kwa 6, Katibu mkuu Zakayo Mjema aliyepata kura 18,
katibu msaidizi akipitaNassoro Mwarizo.
Nafasi
ya Mweka hazina ikienda kwa Omary Nyambuka, Huku nafasi ya Mjumbe wa mkutano
mkuu wa TFF Issa Hamisi alimshinda Athumani Mhando kwa kura 13 kwa 8, na nafasi
ya kamati tendaji ya ARFA ikienda kwa Soud
Abdy.
Washiriki
ambao ni wajumbe wa vyama vya soka kutoka Mkoani hapa waliojitokeza ni kutoka
Arusha Mjini, Monduli, Arumeru, Karatu, Longido, FRAT ambao walifanya jumla ya
wajumbe 19 waliopiga kura.
Huku
nafasi ya wajumbe watatu wa kamati tendaji iliyopata mtu mmoja
na mwakilishi wa vilabu ambazo hazajajazwa utafayika uchaguzi
mdogo baada ya siku 90 kupita alisema katibu wa kamati ya Uchaguzi
Seleimani Kirua.
Katibu
mkuu mpya wa ARFA Zakayo mjema akiongea na gazeti hili alisema
wameingia madarani huku kukiwa na deni
kubwa la kuitendea haki Arusha ili kuweza kurudisha timu ligi
kuu.
"
Kwanza nashukuru nimechuguliwa kwa idadi kubwaya kura na hii ni dhahiri wajumbe
wameniamini na nitahikisha tunashirikiana kwa pamoja na wilaya zetu katika
kuhakikisha soka la mkoa huu linarejea kama ilivyokuwa zamani,"alisema
Mjema.
Mwenyekiti
mpya Peter Temu aliwasihi wadau wa soka wawe na matumaini kuwa mpira utarejea
kulingana na safu mpya yenye morali ya wa kusaidia na kuendeleza
mpira.
Post a Comment