Serikali Kuwapatia Vijana Stadi za Kazi ili Washiriki Kwenye Uchumi wa Viwanda
............................
Na Fatma Salum-MAELEZO
Serikali imepanga kutumia bilioni 15 kuwapatia vijana
stadi za kazi zitakazowawezesha kujiajiri na kushiriki katika ujenzi wa uchumi
wa Viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam wakati wa
kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es
saalam (DIT) na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Akizungumzia
makubaliano hayo Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki
amesema kuwa yatasaidia kuiwezesha Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa vijana hasa
ya kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi ili waweze kushiriki katika ujenzi wa
uchumi wa viwanda.
“Vijana 1000 wataanza
kupata mafunzo mwezi Februari mwaka huu na yatakayohusu utengenezaji wa bidhaa
za ngozi na program hii ipo ndani ya mpango wa miaka mitano.” Alisema Msaki.
Mafunzo hayo ya stadi
za kazi kwa vijana yatagharimiwa na Serikali na yatahusisha vijana walio katika
mfumo rasmi na wale wasio katika mfumo rasmi wa elimu lengo likiwa ni
kuwakwamua vijana ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Akifafanua Msaki
alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuwawezesha vijana baada ya mafunzo hayo
kujiajiri na kuwaajiri wenzao hivyo kuondokana na tatizo la ajira na kuongeza
nguvukazi ya taifa kwenye uzalishaji.
Kwa upande wake Mkuu
wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba alibainisha
kuwa Taasisi hiyo imejipanga vyema kuwawezesha vijana kwa kutoa mafunzo
yanayoendana na mahitaji ya soko na kuweka msisitizo katika mafunzo kwa
vitendo.
Taasisi ya Teknolojia
Dar es salaam (DIT) ipo imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya
Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati.
Post a Comment