Wanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Wajiunga na PSPF
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan uchangiaji wa hiari, (PSS), mwishoni mwa seina ya mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Baada ya semina hiyo wanasheria hao zaidi ya 35 walijiunga na Mfuko huo kupitia mpangio huo wa PSS.
.............................
.............................
Na Khalfan Said
WATUMISHI
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, wamejiunga na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya siku mbili
iliyomalizika leo Januari 4, 2017.
Semina
hiyo iliandaliwa na Mfuko huo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makodna, kutaka wanasheria wa ofisi yake, wapewe semina ili kuwajengea
uwezo wa kutatua kero za wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaofika
Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa shida zinazohusiana na masuala ya Mafao na
Pensheni.
Katika
senmina hiyo iliyoanza Januari 3, 2017, wanasheria hao walipatiwa ufafanuzi wa
kina kuhusu shughuli namajukumu yanayotekelezwa na PSPF.
Meneja
wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni
pamoja na kutambua na kusajili wanachama
wapya, kukusanyan michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama,
kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.
Shughuli
nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa
mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya
ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu,
aliongeza Bi. Magimbi.
Pia
wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni
Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa
uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao
watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari.
Aidha
faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw.Haji
Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya,
mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa
wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la
mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya.
Akifunga
semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria
hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia
kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Huko
mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine
hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia
busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw.
Mayingu.
Aidha
mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo
imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na
kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria
hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.
Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama.
Afisa wa idara ya Pensehni ya Mafao wa PSPF, Bw.Andrew Dayson akitoa mada.
Kaimu Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko huo, Bi.Sophia Mbilikira, akielezea faida za kuwa mwanachama kupitia uchangiaji wa hiari.
Baadhi ya washiriki (wanasheria), wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa PSPF.
Baada ya kuelewa "somo" hatimaye ilifika wakati wa wanasheria hao kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), na hapa wanajaza fomu.
Obote Simon, akikabidhiwa kadi ya kujiunga na uanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS, kutoka kwa Kaimu Meneja wa PSS, Bi. Sophia Mbilikira.
Bw. Mahfoudh K. Mohammed (kushoto), akipokea kadi yake.
Post a Comment