Mkuu wa Wilaya ya Ikungi MIRAJI MTATURU aagiza Kaya kupanda Miti 10 kwa Mwaka
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida, Miraji Mtaturu akizungumza na watendaji wa Wilaya hiyo
na wananchi baada ya kuzindua upandaji miti.
.....................................................................
MKUU wa wilaya ya
Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ameziagiza kaya zote zilizopo katika
wilaya hiyo kupanda miti 10 kwa mwaka na kuitunza ili kukabiliana na ongezeko
la joto la dunia.
Agizo hilo
linahusisha pia vijiji na taasisi zilizopo wilayani humo.
Akizungumza baada
ya uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika katika shule ya sekondari ya
Unyahati mkuu wa wilaya huyo alisema lengo la wilaya ni kupanda miti
550,000 kwa mwaka.
"Naelekeza
kila tarafa kuwa na kitalu cha miche ya miti ili iwe rahisi wananchi kupata
miche na kutimiza lengo tulilojiwekea",amesema Mtaturu.
Mbali na hilo ameitaka
halmashauri kuweka sheria ndogo ili kusaidia utekelezaji wa mipango ya
idara ya misitu waliyojiwekea.
Ametaja changamoto
iliyopo katika utunzaji wa mazingira kuwa ni ufugaji holela na ukame na
kuwataka wananchi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya
maji.
Mtaturu amewapongeza
wadau wa mazingira kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika utunzaji wa
mazingira.
Kauli mbiu ya
uzinduzi huo ni panda miti ikutunze ambapo katika uzinduzi wamefanikiwa
kupanda miti ipatayo 2500.
Mkuu wa wilaya ya
Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akipanda mti katika shule ya sekondari
Unyihati wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika
leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.
Mkuu wa wilaya ya
Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akishirikiana na Kaimu Afisa misitu wa Wilaya
hiyo Bosco Ndunguru kuweka udongo kwenye mti alioupanda katika shule ya
sekondari Unyihati wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya
uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.
Mkuu wa wilaya ya
Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akimwagilia maji kwenye mti alioupanda katika
shule ya sekondari Unyihati iliyopo wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa wa
upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda
miti ikutunze.




Post a Comment