Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka " UDART " yabadili Maisha ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
WAKAZI wa jiji la Dar esSalaam, wameendeela kufaidi mfumo mpya wa usafiri wa umma, (Public Transport), wakitumia mfumo mpya wa usafiriwa mabasi yaendayo kasi yaani UDART.
Mabasi hayo kwa awamu hii yakwanza yanaanza safari zake, kutoka Kimara mwisho hadi Posta yakipitia barabara ya Morogoro. Mabasi mengine hufanya safari zake kuanzia Posta kuelekea Kinondoni pale Morocco yakipitia barabara hiyo hiyo ya Morogoro na kisha kupinda pale Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.
Kamera yetu leo imeangazia jinsi mabasi hayo yanavyotumia njia hizo, pichani moja ya mabasi hayo yenye muundo wa yale ya zamani kwa walioenda "Umri kidogo" watakumbuka mabasi ya Ikarus yaliyokuwa yakitoa huduma za usafiri jijini Dar es Salaam.
Basi hilo liko njiani kuelekea Kimara kupitia Ubungo.
|
Moja ya Basi hilo likiwa kwenye Safari zake za Kawaida Mapema Hii leo. |
Post a Comment