Header Ads

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA 4 LAANZA RASMI

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri , Shindano hili litaruka katika  Runinga ya ITV Kila siku kuanzia 2.08.2015 -21.08.2015 saa 12 Jioni.

 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa hapo jana katika kijiji cha Makumbusho.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisarawe Bw. Ellioth Phillemon akiwakaribisha washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani Kisarawe.
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu. 
  Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo.
 Stephen Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura  ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
  Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi.
 Wanao onekana Mbele ni Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa mama shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini.
 Baadhi ya wageni waalikwa katika Sherehe hizo
 za kuwakaribisha Washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa chakula linalo endeshwa na Shirika la Oxfam katika Kampeni yao ya Grow.

No comments

Powered by Blogger.