“MESI WA SIMBA ATUA COASTAL UNION”
Kulia ni winga mpya wa Coastal
Union Ibrahim Twaha ” Messi” akisaini mkataba wa miaka miwili wa
kuitumikia Coastal Union kulia ni Katibu Mkuu,Kassim El Siagi kushoto ni
Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai.
Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia,Ibrahim Twaha.
……………………………………
Na Mwandishi wetu, TANGA
TIMU ya Coastal Union ya Tanga
imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili kujiimarisha vilivyo katika
safu mbalimbali ambapo jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia
timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili aliyekuwa winga wa kulia wa
Simba,Ibrahim Twaha “Messi”.
Utiliaji saini wa mkataba huo
ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mjini hapa na kushuhudiwa
na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu Kassim El Siagi na Meneja wa
timu hiyo,Akida Machai.
Akiuzngumza mara baada ya
kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi
alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa
aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani.
Alisema kuwa winga huyo ana vitu
adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa
katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo katika
msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
“Niseme tu safari hii
tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka
Tanzania bara na hili tunalifanya kuhakikisha tunarudisha kombe mkoani
hapa ambalo tulilichukua mwaka 1988 “Alisema El Siagi.
Kwa upande wake,Ibrahim Twaha
“Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo alihaidi kuipa mafanikio timu
hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za kuwania
Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Sasa ni kama nimerudi nyumbani
kwa sababu awali nilikuwa naitumikia timu hii hivyo najisikia faraja
kubwa kurudi tena Coastal Union mi nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la
kuipa mafanikio “Alisema Messi.
Awali akizungumza,Meneja wa
Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiri
kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa ubingwa na kurudisha
makali yao ya miaka ya nyuma.
Post a Comment