KIONGOZI WA TALEBAN AHISIWA KUFARIKI DUNIA
Mullah Mohammed Omar, Kiongozi wa Taleban |
Serikali ya Afghanistan inachunguza ripoti za kifo cha kiongozi wa kundi
la Taliban, Mullah Mohammed Omar. Msemaji wa rais wa nchi hiyo
ameyasema hayo kufuatia uvumi uliozagaa kuhusu kifo cha kiongozi huyo wa
waasi.
Wanamgambo wa Taliban wenyewe bado hawajatihibitisha rasmi kifo cha
Mullah Omar, ambae hajaonekana hadharini tangu uvamizi wa majeshi
yalioongozwa na Marekani 2001, ambayo yaliiondoa serikali ya Taliban
mjini Kabulu.
Uvumi wa kuugua kwake, na hata taarifa za kifo zilitapakaa katika
kipindi kilichopita. Ripoti ya hivi karibuni inatolewa siku mbili tu,
kabla duru ya pili ya mazungumzo kati ya wanamgambo wa Taliban na
serikali kufanyika.
Tangazo la msemaji wa rais, Sayed Zafar Hasheemi
linatolewa kwa vyanzo ambavyo havikutambulishwa kutoka upande wa
wapiganaji wa Taliban na serikali kuvieleza vyonzo vya habari, kikiwemo
cha AFP kwamba kiongozi wa Taliban, alikuwa kapoteza uwezo wa kuona wa
jicho moja kafariki dunia miaka miwili au mitatu iliyopita.
Post a Comment