WILAYA ZA ARUSHA ZAONGOZA KWA WAGONJWA WA TRAKOMA
Mratibu wa Mpango wa
kitaifa wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele dkt. Upendo
Mwingira, akionesha fulana yenye ujumbe wa kutokomeza magonjwa hayo
toka shirika lisilo la kiserikali la nchini Marekani la Ending Negleted
Diseases,walokuja nchini tanzania kwa ajili ya
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoani Arusha.
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoani Arusha.
Mratibu wa Trakoma
toka hospitali ya KCMC Patrick Masae akifanya uchunguzi wa macho kwa
wananchi wa kata ya Sinya na Tinga Tinga wilayani Longido.
Wanafunzi wa shule ya msingi sinya wakiwaonesha
wageni (hawapo pichani) jinsi wanavyotumia kibuyu mchirizi kwa kunawa
hii ni mojawapo wa mkakati wa usafi wa mazingira na kuimarisha usafi wa
kunawa mikono na usi kutokomeza ugonjwa wa trakoma, upat.
…………………………………………………………………………………………………………….
Wizara ya afya na ustawi wa jamii itawafanyia upasuaji au urekibishaji wa vikope watu zaidi ya laki tano nchini hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na mratibu wa kitaifa wa mpango wa magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt.Upendo Mwingira kijijini hapa wakati
aliwapokea wageni toka shirika lisilo la kiserikali la Ending Neglected
Disease toka nchini Marekani.
Dkt.Mwingira alisema zoezi hilo la upasuaji limepangwa kufanyika
mwezi wa kumi na litatekelezwa na halmashauri zenye kukabiriwa na
wagonjwa wa Trakoma.
Aidha,alizitaja wilaya za longido,monduli na ngorongoro
zinakabiliwa na wagonjwa wengi wa trakoma kutokana na ukame na mazingira
waishiyo wananchi hao.
“inakadiliwa watu Wapatao laki moja nchini wanahitajika
kufanyiwa urekibishaji wa vikope, na hii ni kutokana na takwimu za
mwisho za mwaka 2014 toka utafiti huo kuanza mwaka 2004″.
Alisema magonjwa haya yanahitaji kutokomezwa hapa nchini ili
kuondoa upofu unaozuilika hivyo wizara inafanya zoezi kila mwaka la
ugawaji wa dawa za’ antibiotics ‘ kwa wananchi wote wa maeneo husika na
kutumia kampeni ya SAFI ambayo ni kusafisha mazingira pamoja na
kuimarisha upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya kunawa uso ili kuzuia
uenezwaji wa trakoma unaonezwa na mbu.
Awali mratibu wa
mradi wa utafiti wa trakoma toka hospitali ya KCMC ambaye ndiye
aliyekuwa akiwafanyia upasuaji wanakijiji hao Patrick Masae alisema
changamoto kubwa inayowakabili wakati wa kuwafikia wananchi wenye
matatizo hayo ni uelewa mdogo, hivyo kushindwa kujitokeza kufanyiwa
upasuaji kwa wakati na hivyo kusababisha uharibifu wa kioo cha jicho na
hivyo wanapofanyiwa upasuaji kwa kuchelewa huamini zoezi hilo si la
kusababisha kuona.
Post a Comment