TAASISI YA KIFEDHA YA BAYPORT YAKABIDHI HUNDI YA MIL 3 KWA WATEGEMEZI WA FAO LA ELIMU MKOANI MBEYA
Alpha Akimu Meneja wa kanda za nyanda za juu kusini akizungumza katika hafla hiyo. |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
TAASISI ya Kifedha ya
Bayport Financial Services, leo jioni imemkabidhi hundi ya Sh Milioni tatu
(3,000,000), Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika
shule ya sekondari Jamsi Sangu iliyopo Vwawa Mbozi Mkoani mbeya , ikiwa ni
sehemu ya mafao yake baada ya mzazi wake kufariki dunia ambaye alikuwa Said mteja
wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao .
Akizungumza katika makabidhiano hayo wilayani
Mbozi mkoani mbeya , Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport
Financial Services, Ruth Bura, amesema mzazi wa mwanafnzi huyo Jaqline Ndyamkama
ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa
mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo leo imemnufaisha
mtoto wake.
Amesema fao hilo la
elimu limekuwa msaada mkubwa kwa wategemezi mara baada ya wazazi kufariki dunia
kwani imechangia kwa kiwango kikubwa wategemezi hao kukamilisha ndoto zao kwa
uhakika zaidio licha ya kufiwa na wqzazi wao.
“Naomba Watanzania wote waweke utaratibu wa
kujiunga na bima hii ambayo malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500
tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000, huku Makato ya bima ya Silver
yakiwa ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh
7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi,” alisema Ruth.
Naye Jaqline
ameishukuru taaasisi hiyo ya Bayport kwa
huduma zao nzuri, huku akisema mafao ya mama yake yatachangia kwa kiasi kikubwa kukamilisha
ndoto zake kwani bado anasafari ndefu katika kufikia malengo ya kielimu huku
pia akiwataka wazazi na walezi kujiunga na utaratibu huo.
Aidha kwa upande wake
bibi mlezi wa Jaqline Ndyamkama ,Angelika Geka , amesema hajawahi kuona taasisi
yenye huduma nzuri kama Bayport Financial Services, hasa baada ya kuhakikishiwa
malipo ya mafao hayo ambayo tayari yamekwisha fanyika malipo ya ada ya mjukuu
wake bila usumbufu wowote, jambo ambalo
ni nadra kwa taasisi nyingi nchini.
Aidha, utaratibu wa
malipo ya huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao umepangwa kulipwa kila
mwaka, ili kuhakikisha kuwa mafao hayo yananufaisha walengwa, hususan kwa wale
wanaoendelea na masomo katika shule na vyuo mbalimbali nchini.
Mwisho.
Post a Comment