|
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Muwakilishi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki
Bw. Jose Castillo, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo ofisini kwake
Migombani. |
|
Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw.
Jose Castillo, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani. |
|
Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw.
Jose Castillo, akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, baada ya mazungumzo yaliyokuwa chini ya
Maalim Seif. Katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Omar Dadi Shajak. |
|
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika
Mashariki, pamoja na baadhi ya watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya
Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR) | | | | | | | | |
...............................................................................
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC)
limesema
litafanya tathmini ya kina kupata njia muafaka za kuisaidia Zanzibar
kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya kwa
jamii.
Hayo yamesema na Kiongozi
wa ujumbe kutoka Shirika hilo, Jose
Vila Del Castillo alipokutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad huko ofisini kwake Migombani na kufanya naye
majadiliano.
Del Castillo amesema kutokana na mazingira ya nchi za visiwa
kama Zanzibar mikakati maalum ya kupambana na dawa na biashara za dawa za
kulevya haina budi kuchukuliwa ili kuwaokoa wananchi wake na kugeuzwa njia za
kusafirishia biashara hiyo haramu.
Amesema msaada huo utalenga zaidi kuipatia Zanzibar vifaa
vya kisasa, kukuza utaalamu kwa watendaji na wadau muhimu wa kupambana na dawa
za kulevya, ikiwemo wendesha mashitaka, wapelelezi, watendaji wa Ofisi ya
Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na wanasheria.
Alisema UNODC litaanza kufanya tathmini hiyo mwezi ujao na
ikikamilika, Shirika hilo litaweza kufahamu ni hatua gani linapaswa kuanza kuzichukua
kwa mashirikiano na Serikali ya Zanzibar kukabiliana na biashara hiyo na
madhara yake.
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali inachukua hatua mbali mbali kuiepusha
Zanzibar kuwa kituo cha kuingizwa na kusafirishiwa dawa za kulevya.
Maalim Seif amesema
juhudi hizo pia zinajumuisha kuwasaidia wananchi wasijiingize kwenye vitendo
vya kutumia au kufanya biashara hiyo, ikiwemo kutoa miongozo kwa makundi mbali
mbali ya jamii, wakiwemo wanafunzi wa skuli mbali mbali.
Kuhusu wale ambao
tayari wanatumia dawa hizo, Maalim Seif amesema Serikali kwa mashirikiano na
jumuiya na watu binafsi imefungua vituo maalum kwa ajili ya kuwasaidia
kubadilisha tabia, ili baadaye wawe raia wema katika jamii yao.
Makamu wa Kwanza wa
Rais amesema hivi sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imeanza ujenzi wa kituo
cha kisasa cha kurekebisha tabia wananchi wanaotumia dawa hizo, ambacho jengo
lake litakuwa na ghora tatu na sehemu zote muhimu kwa mahitaji yao.
Hata hivyo, alisema
zipo baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya dawa za
kulevya Zanzibar, ikiwemo uhaba wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na ukaguzi
katika maeneo ya kuingilia na kutokea nchini.
Changamoto nyengine
alizozitaja ni mazingira ya visiwa vya Zanzibar kuwa na bandari nyingi
zisizokuwa rasmi ambazo hutumiwa na baadhi ya watu kuingiza vitu vyenye madhara,
zikiwemo dawa za kulevya.
Katika
mazungumzo hayo, Mshauri wa masuala ya Ukimwi wa Shirika hilo Kanda ya Afrika
Mashariki, Sylvie
Bertrand
amesema msaada huo wa UNODC pia utajumuisha kuimarisha mazingira ya vyuo vya
mafunzo, ili kuepusha maambukizi ya ukimwi na athari nyengine zitokanazo na
dawa za kulevya.
Post a Comment