SERIKALI YASAINI MKATABA WA KUKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 12
Baadhi
ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA wakati wa hafla ya
kusaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya mapato ya ndani kwa mwaka wa
fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.
(Habari Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
……………………………………..
Serikaki imesainiana Mkataba wa
Makubaliano ya kukusanya Sh. Milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.
Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dar es Salaam
kati ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu kwenye
hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya
Fedha na TRA.
“Hakikisheni mnakusanya mapato kama ilivyopangwa na kufikia
malengo tuliyojiwekea katika kukusanya mapato ya ndani katika mwaka huu
wa fedha” alisema Waziri wa Saada.
Waziri huyo aliwaasa watendaji wa TRA kuwawekea wafanya kazi
mazingira mazuri ya kutekeleza wajibu wao inavyopaswa na wanapokwenda
kinyume na makubaliano ya kazi watawajibishwa kwa mujibu wa sheri,
kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA Bernard
Mchomvu alimhakikishia Waziri wa Fedha kuwa watafikia lengo
walilokubaliana kukusanya na hata kuzidi kiwango hicho ambacho
kimeainishwa katika bajeti ya Serikali.
Post a Comment