RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot
alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya
kiongozi huyo jijini Sydney.
– Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na
Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe
28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia
Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya
kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku
akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika
makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot
alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai, 2015 katika makao Makuu ya
kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba la serikali jijini
Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na
Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.
PICHA NA IKULU
………………………………………………………
Waziri Mkuu wa Australia,
Bwana Tony Abbot amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua
kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba nchini
Tanzania.
“Nakupongeza sana kwa
uamuzi wako wa kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la
nadra sana Barani Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani namna
hii” Bw. Abbot amemuambia Rais Kikwete na kumueleza awe na uhakika kuwa ” Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kukuza uchumi” ameongeza.
Rais Kikwete na Waziri Mkuu
Abbot pia wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana
katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa
kidiplomasia, kiuchumi na kijamii.
Rais Kikwete yuko nchini
Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa
Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.
Rais Kikwete amepokelewa leo
asubuhi tarehe 28 katika makao Makuu ya kiongozi wa Australia kwa
heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha
mchana na baadae kupanda mti kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya
nchi hizi mbili kwa kipindi kirefu kijacho.
Tanzania na Australia
zimedumu katika ushirikiano baina ya nchi zao tangu miaka ya sitini na
sasa nchi mbili hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya zaidi katika
sekta mbalimbali zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.
Baadae leo jioni Rais Kikwete
atakutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza
nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta
mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inaweza kunufaika kutokana na
kupata gesi.
Tayari Serikali ya Australia
na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika
vyuo vya ufundi stadi VETA na tafiti mbalimbali katika Kilimo.
Kesho tarehe 29 Julai, 2015
Rais Kikwete anatarajia kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya
Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa
katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini
Tanzania na Dunia kwa ujumla.
Rais Kikwete anatarajia
kuondoka Australia na kurejea Tanzania baada ya shughuli ya kupokea
shahada yake na ratiba yake kwa ujumla.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Canberra-Australia
28 Julai, 2015
Post a Comment