FILAMU YA " I SHOT BI KIDUDE" KUONESHWA TAMASHA LA ZIFF
‘Makala ya Kusisimua
yenye matukio yenye hisia nzito.’
Andy Markowitz, Tovuti ya Muziki wa Filamu Music Film Web
‘Tafakari ya
kusisimua ya urafiki usio wa kawaida kati ya Kijana Mtengenezaji wa filamu na
diva wa Zanzibar mzee wa miaka 100 Zanzibar diva’ Garth
Cartwright - mwandishi, “More Miles Than Money”Umbali mkubwa kuliko fedha”
Martin Mhando, Mkurugenzi ZIFF
Nilimpiga Picha Bi
Kidude “I Shot Bi Kidude”, ni makala mpya ya simulizi iliyotayarishwa na Andy Jones, mtengenezaji
wa filamu wa Uingereza ambayo
itahitimisha Tamasha la Filamu la Kimataifa hapa Zanzibar,. Watazamaji wa
Zanzibar watamsikia msimulizi mwenyewe akisimulia kwa lugha ya Kiswahili ambayo
alijifunza kwa muda mfupi matamshi kwa msaada wa wanamziki Wazanzibari Mim
Suleiman na Bwana Mohammed Issa Matona.
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne, kuanzia 2003 mpaka
2006, Andy Jones alimfuata Bi Kidude
alipokuwa akisafiri duniani. Matokeo yake ni kupokea tuzo ya filamu AS OLD
AS MY TONGUE, ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika mwaka
2006 na baadaye iliendelea kuwa kivutio kwenye matamasha ya filamu na
muziki duniani kote..
Baada ya kutembelea Zanzibar kila mwaka kwa karibu muongo
mmoja, Jones hakuweza tena kumuona Bi Kidude kwa muda wa miaka mitatu.
Katika mwezi Agosti mwaka 2012, taarifa zilifika Uingereza zikieleza kuwa
mwanamziki kinara maarufu Africa Mashariki ametekwa nyara . Haikuchukua muda
mrefu Andy alirudi Zanzibar kupata ukweli wa taarifa .
Wiki chache tu baada ya kisa hicho kuibuliwa kwa picha
zilizopigwa na Natalie Haarhoff kutoka Afrika ya Kusini , muimbaji mzee sana wa
kimataifa amefariki, akiwa na umri unaosemekana kuwa zaidi ya miaka mia moja
. Jones alikurupuka kutoka nyumbani kwake huko Newcastlena kufika uwanja
wa ndege wa Heathrow dadikia chache kabla ya ndege iliyopangwa kwenda Nairobi
kuondoka. Alifika kwenye mazishi ambayo yalishtua kisiwa kizima..
“I SHOT BI KIDUDE, ni simulizi yangu kuhusu mambo
yalivyokuwa wakati wa mwisho wa maisha ya
Bi Kidude’ . Kama ilivyo kwenye simulizi nyingine , kuna maelezo
mbalimbali kuhusu ukweli wa jambo. Kimsingi kuna vitu vingine ambavo si
rahisi kwa mgeni kuvitambua, hata hivyo ninatumaini kuna vitu vingine haviwezi
kufichika machoni . Ninaloona mimi hisia ya kusherehekea nguvu za muziki na
kufanya vitu ambavyo vinatuletea furaha
pale tunapoweza ” Andy Jones anasema.
Post a Comment