MEYA KAPUNGA KUTETEA KITI CHAKE CHA UMEYA JIJI LA MBEYA
Na Mwandishi wetu,Mbeya
ALIYEKUWA Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga ametangaza kutetea nafasi yake ya kiti cha udiwani kupitia Kata ya Itiji ndani ya Jiji la Mbeya.
Ujio wa
Kapunga tena, umeonyesha kuwashtua wananchi wa eneo hilo pamoja na baadhi ya
wakazi wa Jiji la Mbeya, ambao kupitia maoni yao walidai kwamba mgombea huyo
alipaswa kupumzika na nafasi hiyo kuwaachia vijana.
Akizungumza
na baadhi ya wananchi wa Kata ya Itiji waliokusanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa CCM wa Kata hiyo, Kapunga alisema ameamua kuitetea nafasi hiyo lengo likiwa
ni kutimiza malengo yake aliyojiwekea ya kuwafikishia maendeleo wakazi wa eneo
hilo.
Amesema,
katika kipindi chote alichokuwepo madarakani, ameweza kutimiza na kutatua
changamoto mbalimbali za maendelei na kubakia asilimia chache ambazo endapo
wananchi hao watampa ridhaa ya kuwaongoza kwa mara nyingine tena basi
atamalizia kipande kidogo kilichobakia.
Amesema,
katika kipindi chote alichobahatika kuwakilisha wanaitiji alifanikiwa kutatua
changamoto mbalimbali kama vile maji, elimu kuboresha miundombinu ya barabara
katika kiwango cha vumbi.
Amesema,
kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya kulitokana na eneo lililopangwa
kujengwa kituo hicho kuwa na mgogoro kati ya watendaji wa halmashauri ya Jiji
na wafanyabiashara wadogo ambao walikuwa wakilitumia eneo hilo kama soko la
wakulima.
Amesema,
wafanyabiashara hao wamekuwa wakiamini kuwa eneo hilo ni halali kwao kwa
kuendeshea biashara zao jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani eneo hilo
lilikuwa ni machinjio ya zamani ya ng’ombe kabla serikali ya kuihamishia eneo
la Veta.
Amesema,
mazungumzo yalikuwa yakiendelea kufanyika jinsi ya kulirudisha eneo hilo na
kubadilisha matumizi kwa kujenga kituo cha afya hivyo anaamini endapo atapatiwa
nafasi nyingine atatekeleza ahadi hiyo ya kuwafikishia karibu huduma ya afya
wakazi wa Itiji.
Aidha, akizungumzia
ujenzi wa barabara katika kiwango cha lami, Kapunga alisema kuwa barabara za
eneo hilo hazikuingizwa kwenye mradi wa barabara uliokuwa ukifadhiliwa na Benki
ya Dunia lakini tayari serikali ilikuwa ikitafuta fedha za kuona ni jinsi gani
barabra za eneo hilo zitaboreshwa kutoka kiwango cha vumbi na kufikia lami.
Hata
hivyo, Kapunga hakusita kuwatupia lawama baadhi ya viongozi wenzake wa chama
cha mapinduzi kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwake jambo ambalo limesababisha
yeye kutupiwa lawama na wananchi wa eneo hilo na wakazi wa Jiji la Mbeya.
JAMII MOJA BLOG
JAMII MOJA BLOG
Post a Comment