MSETO WA TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hatua ya nusu Fainali ya Michuano
ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup)
inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa Taifa, huku kiingilio cha
chini katika michezo hiyo kikiwa ni shilingi elfu tatu (3,000).
Viingilio vingine vya michezo
hiyo ya kesho ni VIP A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B
& C, Shilingi elfu kumi (10,000) na sehemu nyingine ya uwanja
iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu,
kijani na rangi ya chungwa.
Timu nne kutoka katika nchi nne
wanachama wa michuano hiyo, Azam FC (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), KCCA
(Uganda) na Al Khartoum (Sudan) zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali
itayochezwa uwanja wa Taifa siku ya ijumaa.
Mchezo wa kwanza utakaonza saa
7:30 mchana utazikutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya itakayocheza dhidi
ya Khartoum ya Sudan, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kufutia
timu hizo kutoka sare katika mchezo wake wa awali hatua ya makundi.
Katika mchezo wa kwanza
uliozikutanisha timu hizo, kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na Frank
Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao 1- 1 ndani ya dakika 90, hali
ambayo inapelekea kufaya mchezow wa kesho kuwa mgumu kwa kila timu
kuhitaji nafasi ya kusonga mbele hatua ya fainali.
Gor Mahia mabingwa mara tano wa
michuano hiyo, wataingia uwanjani kusaka ushindi ili kusonga hatua ya
fainali ili waweza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita, sawa na klabu ya
Simba inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo.
Kocha Frank Nuttal atakua
akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid Alucho, Kagere Meddie, Michael
Olunga, Sibomana Abouba, Karim Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi, Nahodha
Musa Mohamed, na mlinda mlango Boniface Oluoch katika kusaka ushindi
dhidi ya Khartoum.
Kwesi Appiah atashuka dimbani
akiwategemea wachezaji wake nyota, Antony Akumu, Dominic Abdui, Samawal
Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba na nahodha Amin Ibrahim.
Vita kali itakua kwa washambulaji
Michael Olunga wa Gor Mahia na Salaheldin Osman wote wenye mabao manne,
wakiwania kuongeza bao katika mchezo huo wa kesho ili kujiweka katika
mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu.
Nusu fainali ya pili
itawakutanisha waoka mikate wa Azam FC dhidi ya Mamlaka ya jiji la
Kampala (KCCA), mchezo utaokanza majira ya 9:45 kwa saa za Afrika na
Kati katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo pia unatarajiwa kuwa
na upinzani mkali kufutia timu hizo katika mchezo wa hatua ya makundi,
Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao liliofungwa na nahodha wake
John Bocco.
KCCA chini ya kocha wake Mike
Mutebi watashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo huo, ikiwa ni
kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza na kupata ushindi utakaowavusha
mpaka katika hatua ya fainali.
Kocha Mutebi atakuwa akiwategmea
wachezaji wake nyota, Nahodha Tom Matiko, Opio Emmanuel, Joseph Ochaya,
Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma, Habib Kavuma na Muzamil Mutyaba.
Azam FC itashuka dimbani kutaka
kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA ya Uganda, na kuweza kukata tiketi
ya kucheza fainali siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Kocha wa Stewart Hall wa Azam
atakua akijivunia safu yake ya ulinzi ambayo haijaruhusu bao tangu
kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga
mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.
Hall atashuka dimbani akiwategema
nyota wake Nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Aggrey Morris, Himid Mao,
Kipre Tchetche, Jean Baptist Mugiranenza, Frank Domayo na mlinda mlango
Aishi Manula.
TFF YAIPONGEZA AZAM FC
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za pongezi kwa klabu ya
Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano
ya Kombe la Kagame inayotimua vumbi jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake kwa uongozi wa
klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na kuongeza bidii katika
hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali na
kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti wawakilishi
pekee wa nchi kwenye michuano hiyo.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira
na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam FC katika mchezo wake
wa kesho wa nusu fainali dhidi ya KCCA.
TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI
Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Moshi Shaban,
kufutia kifo cha Moshi kilichotokea jana jijini Dar s salaam na mazishi
kufanyika leo jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake za rambirambi
kwa familia ya marehemu Moshi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na
marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na
kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa
Marehemu Moshi Shaban ni baba wa
wachezaji waliowahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Haruna Moshi
“Boban) na Iddy Moshi (Mnyamwezi).
TFF YAANDAA KOZI YA WAAMUZI WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2015/2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa kozi ya waamuzi wa mpira
wa miguu watakaochezesha mechi za
Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza 2015/2016, kozi hiyo itafanyika
jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21 -24/08/2015.
Washiriki wa kozi hii ni waamuzi
waliochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza msimu wa
2014/2015 wenye umri wa miaka 21 – 45 kwa wanawake na
miaka 23 – 45 kwa wanaume.
Waamuzi wote wanatakiwa kuripoti
tarehe 21/08/2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume Ilala Dar es
salaam na wawasilishe vyeti halisi vya kuzaliwa na nakala zake.
Pamoja na cheti cha kuzaliwa kwa
kila mwamuzi ni lazima alete kadi ya kupigia kura au passport ya
kusafiria kwa ajili ya uthibitisho wa umri wake.
Washiriki wa kozi watafanya
mitihani ya kupima afya, utimamu wa mwili na sheria za mpira wa miguu
Trivia (kuandika), video clips (offside na match analysis).
Waamuzi watakaofaulu watashindanishwa kupata waamuzi arobaini (40) na
waamuzi wasaidizi sabini (70) watakaochezesha Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza
kwa msimu wa 2015/2016. Shirikisho linawatakia wote maandalizi mema.
Baada ya kozi ya waamuzi kutakuwa
na kozi ya makamisaa wa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza
ambayo itafanyika kuanzia tarehe 24/08/2015 hadi tarehe 25/08/2015.
Makamisaa wote wanatakiwa
kuripoti tarehe 23/08/2015 saa 10:00 alasiri uwanja wa Taifa, Makamisaa
watakao husika na kozi hii ni wale wote walio simamia michezo ya Ligi
Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2014/15.
Makamisaa watafanya mtihani wa
sheria za mpira wa miguu (Trivia, offside, match analysis) na kupima
mwamuzi anapochezesha (evaluation). Wale watakaofaulu ndiyo
watakaopangwa kusimamia michezo hiyo.
Post a Comment