WAZIRI WA ELIMU DKT. SHUKURU KAWAMBWA APATA MPINZANI JIMBO LA BAGAMOYO
Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew
Juma Salum Yangwe.
Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew
Juma Salum Yangwe (katikati), akizungumza na makada na wanahabari wakati akitangaza nia mjini Bagamoyo mkoani Pwani Pwani jana. Kushoto ni Meneja wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe na Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga.
Meneja wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mzee Abdallah Ngumbe akizungumza katika mkutano huo na wakati akimpa ushauri mbalimbali mtangaza nia huyo.
Profesa Sameheni Kejeli akizungumza katika mkutano huo.
Mzee Hussein Lugome akizungumza katika mkutano huo.
Mama mzazi wa mtangania huyo, Mary Yungwe akiwasalimia makada wa CCM katika mkutano huo.
Mtangaza nia huyo akipongezwa na vijana baada ya mkutano huo.
Pongezi zikiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Mtangazania huyo akiwa na wadau wake.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa amepata mpinzani baada ya kijana mdogo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Yungwe kutangaza nia ya ubunge katika jimbo hilo.
Akizungumza na makada wa CCM na waaandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana, Yungwe alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kusukuma maendeleo ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu.
"Wanaccm wenzangu na wazee wangu nimeamua kugombea nafasi hii ili niwatumikie kwani Bagamoyo naelewa vizuri na nitaendelea kuwa wilayani hapa ili tushirikiane katika mambo mbalimbali ya nmaendeleo" alisema Yungwe.
Yungwe alisema mambo atakayoyapa kipaumbele ni matatu, uchumi, Afya na Mawasiliano na kuwa hata penda aitwe mbunge bali aitwe mratibu na kuwa atakuwa na ofisi yake ya ubunge katika wilaya hiyo kwa lengo la kuwa jirani na wananchi zaidi.
Alisema maeneo mengine atakayoyafanyia kazi kwa kushirikiana na wananchi ni pamoja na kuinua uchumi wa jimbo hilo kupitia uvuvi, kuweka mipango mizuri ya kukusanya fedha kupitia viwanja vya michezo, utalii na mapato yatokanayo na uwekezaji na ujenzi wa soko la kisasa.
Alisema pia atashughulikia migogoro ya ardhi katika maeneo yote ya jimbo hilo yakiwemo ya Zinga na Pande ambayo inapunguza kasi ya maendeleo ya wananchi katika jimbo hilo.
Yungwe alisema kauli mbiu yake ni "Fikiri Tofauti, Badilika kwa Maendeleo Endelevu ya Bagamoyo.
Jimbo la Bagamoyo katika kpindi cha miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa lilikuwa likiongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Post a Comment