Header Ads

AMON MPANJU AJITOSA KUGOMBEA JIMBO LA KAWE

Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju ambaye pia alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mpya amejitokeza hii leo sambamba na wana CCM wengine katika safari ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kawe Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na Father Kidevu Blog, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Mpanju amesema huu ni wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Kawe.

Mpanju ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, amesema wanakawe wananafasi sasa ya kuandika historia  ya aina yake si tu kumchagua mtu mlemavu bali kumchagua, kijana na mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa kawe na taifa.

“Huu ni wakati wa wananchi wa Kawe kuandika historia ya aina yake, si tu  kwa kumchagua mtu mwenye ulemavu kuwaongoza bali kijana mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi yua wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Mpanju.

Mpanju amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa 39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akizungumza na wanahabari, Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe akimsaidia kutia saini ya dole gumba Mpanji.
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe, kwaajili ya  kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kumteua kugombea Ubunge Jimbo la Uchaguzi la Kawe katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. 
Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (pichani), amempongeza Mpanju kwa uamuzi wake huo na kusema kuwa anatekeleza moja ya kanuzi na sheria za Chama kuwa watu wote ni sawa na walemavu wanahaki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa vipongozi.

“Mimi nitoe wito kwa watu wote wenye ulemavu nchini ambao wanasifa na vigezo vinavyotakikana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini wajitokeze na kufanya hivyo na watatendewa sawa sawa na wengine bila ubaguzi au unyanyapaa,”alisema Sheshe.

No comments

Powered by Blogger.