TANZANIA YAFANYA KUFURU MBIO ZA NYIKA SARPCCO
Wanariadha wa mbio za nyika katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) wakiendelea na mbio hizo jana katika mji wa Mbabane Swaziland ambapo wanariadha wa Polisi Tanzania walifanikiwa kushika nafasi tatu za mwanzo.
(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)
Wanariadha wa mbio za nyika kutoka Polisi Tanzania
wakipongezana baada ya kumaliza kukimbia mbio hizo jana katika mji wa
Mbabane Swaziland ambapo michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini
mwa Afrika(SARPCCO) inaendelea Tanzania walifanikiwa kushika nafasi
tatu za mwanzo katika mbio hizo.
………………………………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland
Wanariadha
wa Polisi Tanzania walioshiriki katika mbio za nyika katika michezo ya
majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini (SARPCCO) wamefanya kufuru kwa
kuzoa medali zote baada ya kushika nafasi tatu za juu.
Wanariadha
waliofanya vizuri na nafasi zao katika mabano ni pamoja na Basili John
(1), Fabian Nelson(2) na Josephat Joshua(3) ambapo mshindi wa
kwanza aliweza kutumia muda wa dakika 29:26:00.
Wanariadha
wengine kutoka Tanzania walioshiriki mbio hizo ni pamoja na Osward
Revelian, Wilbado Peter, Silvester Naal na Fabiola Willium kwa upande wa
wanawake na hivyo kusababisha ushindi wa jumla kwa kupata medali ya
dhahabu.
Kwa matokeo
hayo timu ya Tanzania inayoshiriki michezo hiyo imefanikiwa kufikisha
medali sita za dhahabu, nne za fedha na mbili za shaba na hivyo
kujihakikishia nafasi nzuri katika ushindi wa jumla wakati michezo hiyo
itakapofikia ukingoni Agosti pili mwaka huu.
Akizungumzia
matokeo hayo Kocha wa Wanariadha hao Rogart Steven alisema wanariadha
hao walijiandaa vyema na kujituma licha ya kukabiliwa na upinzani mkubwa
kutoka kwa wanariadha wa Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.
Katika
Michezo ya Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Wanariadha kumi na mbili
pekee ambao wameonyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo ukilinganisha
na mataifa mengine ambayo yameleta idadi kubwa ya wanamichezo.
Post a Comment