STARTIMES YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA SHULE YA MSINGI MAALUMU YA AIRWING JIJINI DAR ES SALAAM
Kutoka kulia ni wafanyakazi wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Elena Liu na Paulina Kaka wakifurahia jambo pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili, Bw. Issa Mkasa wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Fabiola Malisa.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (mwenye hijab) akikabidhi moja ya msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Airwing, kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakishuhudia tukio hilo kutoka wa pili kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa na Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kitengo maalum cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo katikati ni Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (mwenye hijab) akikabidhi moja ya msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Airwing, kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakijumuika pamoja naye katika tukio hilo wa pili kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa na wa pili kushoto ni Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.
Na Mwandishi Wetu
Serikali
yaombwa kutilia mkazo kuhakikisha kila shule ya msingi inakuwa na kitengo
maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa viungo mbalimbali ili kuwapatia na wao
fursa ya kupata elimu.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa wakati wa
kupokea msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kutoka kwa wafanyakazi wa
kampuni ya StarTimes Tanzania kwa ajili ya kitengo maalumu cha wanafunzi wenye
ulemavu wa akili.
Bi.
Malisa alisema kuwa shuleni kwake wanacho kitengo cha kuwafundisha wanafunzi
wenye ulemavu wa akili ambao kwa sasa wapo jumla ya 65, wanafunzi 20 ni
wasichana na wanafunzi 45 ni wavulana.
“Hapa
kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili ukiachana na wanafunzi
wengine wa kawaida. Kwa sasa tunalo darasa moja ambalo tunawafundishia kwa
kupeana amu na wanafunzi wa darasa la pili. Yaani wao wanaingia asubuhi na kutoka
saa tano baada ya hapo wanafunzi wengine hulitumia hilo darasa. Tumeamua
kufanya hivi kutokana na uhaba wa madarasa wenyewe.” Alisema Bi. Malisa
“Kuanzishwa
kwa kitengo hiki lengo ni kuwafundisha watoto hawa wenye ulemavu wa akili nao
waweze kupata stadi mbalimbali za kujumuika pamoja na jamii inayowazunguka.
Jamii hudhani kuwa motto akizaliwa na ulemavu wa aina yeyote ile anakuwa ni mtu
tegemezi. Sisi tunakanusha suala hilo kwani tunao hapa ambao tunawafundisha na
wengi wameonyesha maendeleo mazuri. Kwa mfano kuna ambao baada ya kumaliza
vipindi darasani hurudi wenyewe majumbani na hata kuja wenyewe shuleni kila
siku.” Alisema na kuongezea Bi. Malisa
“Sisi
kama uongozi wa shule tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuwasaidia watoto hawa
ili wajitambue na kuweza kuishi na jamii. Na tumefanikiwa kwa hilo, kwa mfano
tunao wanafunzi wawili ambao baada ya kufundishwa kwenye kitengo hiki na
kuonyesha maendeleo mazuri wamejiunga na wanafunzi wa kawaida, mmoja yuko
darasa la saba na mwengine la nne,” alisema na kuongezea Mwalimu Mkuu, “Na tena
wanasoma bila shida yoyote na wanafunzi wengine wamewazoea wanasoma pamoja
nao.”
“Changamoto
kubwa tunayokumbana nayo nib ado tuna uhaba wa madarasa kama nilivyoelezea
awali tunatumia darasa kwa awamu. Kwani wao wanahitaji muda zaidi tofauti na
wanafunzi wa kawaida. Japokuwa tunapokea msaada kutoka serikalini, kwa
makampuni na taasisi zingine bado hautoshi. Tunaomba serikali itilie mkazo
zaidi kwa kila shule kuwepo na kitengo cha namna hii kwani hali hiyo itapelekea
wazazi kutowaficha watoto majumbani. Pia vituo hivi huwapunguzia wazazi mzigo
mkubwa wa kuwalea kwani huwa salama mahali hapa na kuwafanya wao kufanya
shughuli zingine za kujenga taifa.” Alihitimisha Bi. Malisa
Naye
kwa upande wake akiongea kwa niaba ya wafanyakazi, Makamu wa Rais wa StarTimes
Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wao kama kama kampuni na watanzania
wameguswa sana na ustawai watoto hawa ambao jamii huwachukilia tofauti.
“Bado
watanzania tunayosafari ndefu ya kubadili mtazamo juu ya watoto wenye ulemavu.
Tunatakiwa kuondoa dhana ya bado kufikiria ukiwa na motto mlevu basi atakuwa
tegemezi kwa maisha yake yote duniani. Ulemavu unatofautiana na ule ambao
unaweza kutibika watoto hawa wasaidiwe. Lakini jambo hili halitowezekana kama
serikali haitojenga vituo hivi kwenye kila shule ya msingi na pia wadau nao
kujitokeza kuziunga mkono.” Alisema Bi. Hanif
“Na
kusema ukweli mahitaji ambayo yanahitajika katika shule hizi yamo ndani ya
uwezo wetu watanzania. Bado tunahitaji mwamko wa kutosha kwani si wazazi wote
wanao uwezo wa kumudu gharama za kuwahudumia watoto wenye ulemavu.
Tumekuja
hapa tumezungumza na walimu wametupa hali halisi kuwa asilimia kubwa ya
wanafunzi hawa uwezo wao ni mdogo hivyo wanahitaji misaada yetu,” alisema na
kumalizia Bi. Hanif, “Hivyo basi kwa msaada wetu huu ambao sisi wafanyakazi wa
StarTimes tumejikusanya na kuutoa, tunatarajia pia makampuni na taasisi
nyingine wataiga na kufanya hivyo. Ni jukumu letu sote kuwasaidia na kuwalea
watoto hawa kwani Mungu ana makusudio yake kuwaumba hivi.”
Msaada
wa wafanyakazi wa StarTimes Tanzania uliotolea kwa kitengo hiko cha wanafunzi
wenye ulemavu wa akili shuleni Airwing ni pamoja na sukari, mikate, majani ya
chai, blueband, chumvi, sabuni za unga na mche, vibiriti, na mengineyo. Msaada
huo umelenga kuwahudumia wanafunzi hao kwa muda ambao wapo shuleni na kwa
wazazi na walezi wa wanafunzi hao.
Post a Comment