TRA YADHAMIRIA KUFIKIA LENGO LA UKUSANYAJI WA KODI
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwaeleza wajumbe wa Bodi ya Taifa ya
wahasibu na wakaguzi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria mpya ya Kodi ya
ongezeko la thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1,
2015 na jinsi itakavyobadilisha baadhi ya mifumo ya kibiashara,wakati wa
Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya
wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.
2- Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya
wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia akimshukuru Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa kuhudhuria ufunguzi
wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa
ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) na kuahidi kuwa washiriki wazuri katika
mabadiliko katika sekta ya Kodi nchini,wakati wa Semina ya pamoja Kati
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi
(NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.
3- Baadhi ya wajumbe wa semina ya
pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu
na wakaguzi (NBAA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akimueleza jambo Mjumbe wa Bodi ya Taifa
ya wahasibu na wakaguzi na mwenyekiti wa Kamati ya sekta ya Umma
Bw.Nicholus Duhia, katikati ni Bi. Diana Masalla Meneja Elimu kwa
Mlipakodi.
Bw. Yona Kilagane akiwasilisha
mada wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na
Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.
…………………………………………………………………..
Na Hassan Silayo - MAELEZO
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imedhamiria kufikia malengo
yake katika ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kufikia shilingi
trilioni 22.3 iliyojiwekea katika bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016.
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade wakati wa Semina ya wahasibu
iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu
na wakaguzi (NBAA) ikiwa na lengo la kujadili kuhusu masuala ya kodi,
bajeti na uchumi kwa ujumla.
“Moja kati ya malengo tuliyojiwekea sisi kama mamlaka ni
kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa mapato tukiwa na lengo la
kuiwezesha kufikia kiasi cha shilingi trilioni 22.3 zilizopangwa
kutumika katika mwaka huu wa fedha” Alisema Bw.Rished.
Akieleza kuhusu sheria mpya ya kodi iliyoanza kutumika julai 1,
2015 Bw. Rished alisema kuwa kuwa sheria hii inategemewa kubadilisha
baadhi ya mifumo ya kibiashara nchini.
Pia alieleza kuwa kitu muhimu kwa sasa ni wajumbe wa bodi hiyo
kukaa na kuipitia sheria hiyo na kuangalia mabadiliko yaliyomo na wao
kama wadau katika sekta hiyo kusaidia katika kuboresha mazingira ya
kibiashara.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus
Duhia alimshukuru Kamishna Mkuu kuhudhuria semina hiyo na kuahidi kuwa
washiriki wazuri katika mabadiliko ya sekta ya Kodi nchini
“Ndugu Kamishna Mkuu, umekuwa ukishirikiana na kufanya kazi kwa
karibu na bodi hii, hivyo tunakuahidi baada ya kumaliza semina hii
tutakuwa washiriki wazuri hasa katika mabadiliko ya sekta ya Kodi
nchini” Alisema Bw. Duhia.
Aidha, Mshiriki wa Mafunzo hayo na muwakilishi kutoka Jubilee
Insurance Bi. Hellena Mzena alisema kuwa kikubwa anachotegemea kujifunza
kutoka kwenye semina hiyo ni jinsi gani sekta ya Bima ilivyoguswa kwa
mara ya kwanza katika Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya
mwaka 2014 na jinsi gani wataenda sambamba na mabadiliko hayo.
Post a Comment