MWENGE WA UHURU WAANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI RUKWA LEO
Mkuu
wa Wilaya ya Momba Richard Mbeho kushoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga Methew Sedoyyeka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng.
Stella Manyanya leo tarehe 11 Julai 2015 tayari kwa kuanza mbio zake za
siku nne Mkoani Rukwa. Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi mbalimbali ya
maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni 11.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akishika Mwenge wa Uhuru ulipowasili Mkoani Rukwa leo tarehe 11 Julai 2015.
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Mkutano Mkoani Rukwa wakiwa wamebeba bendera
ya taifa kwa ajili ya kuipeleka na kuipeperusha eneo la makabidhiano ya
Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda Mkoa wa Rukwa.
Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akishika mwenge wa Uhuru baada ya
kuwasili Mkoani Rukwa leo.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Juma Khatibu Chum akikata utepe
kuashiria kuzindua rasmi mradi wa maji ya mserereko katika kijiji cha
Kamnyazia Wilayani Sumbawanga leo katika ziara ya mbio za mwenge wa
Uhuru Mkoani Rukwa.
Sehemu ya wananchi wakishuhudia mwenge wa Uhuru Mkoani Rukwa leo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
Post a Comment