TAKUKURU YAKANUSHA TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA NAPE
Steven Chami, Kamanda wa Takukuru mkoa wa Lindi
*Yasisitiza hiyo ni michezo michafu ya kisiasa.
*Yavitaka vyombo vya habari kuwa makini
Na Mwandishi Wetu. Lindi
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Lindi imekanusha
tuhuma rushwa dhidi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape
Nnauye zilizoandikwa na baadhi ya magazeti ya leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya Ofisi yake, Kamanda wa Takukuru mkoa wa
Lindi Ndugu Steven Chami amefafanua kuwa kilichofanywa jana ilikuwa ni
kujiridhisha na viwango vya fedha vinavyotolewa na wanasiasa wote
walioomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali mkoani humo.
Ndugu
Chami alisema Ndugu Nape ni miongoni mwa wanasiasa wanaoomba ridhaa ya
ubunge kupitia CCM katika jimbo la Mtama mkoani Lindi na kwamba kwa kuwa
alikuwa ni miongoni mwa wanasiasa aliyeingia katika benki ya NMB mjini
Lindi jana ili kutoa fedha ilikuwa si jambo la busara kuacha aende bila
kujiridhisha na kiwango pamoja na matumizi ya fedha husika alizokuwa
akichukua.
Hata
hivyo Kamanda huyo wa TAKUKURU alisisitiza kuwa baada ya kumuomba Ndugu
Nape kuongozana naye ofisini kwake kwa mahojiano ambayo yalichukua kati
ya dakika 30 na 45, alijiridhisha kuwa kiwango cha fedha alichokuwa
amechukua benki ni cha kawaida.
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo wa TAKUKURU, Ndugu Nape alichukua benki jumla ya
shilingi Milioni Tatu ambazo alitaka kuzitumia kwa ajili ya kuwalipa
Mawakala wake 156 ambao aliwaandaa kusimamia zoezi la upigaji kura
katika vituo vyote jimboni humo, na kwamba kiasi hicho cha fedha
kilikuwa pungufu hata ya uhalisia wa mahitaji yake.
Ndugu
Chami amevitaka vyombo vya habari kuwa makini katika kuripoti habari
zake na kuepuka upotoshaji kama huo uliofanywa na magazeti ya leo ya
Nipashe, Mtanzania, Majira na Tanzania Daima jambo ambalo linajenga
dhana inayobeba dhamira na malengo mabaya dhidi ya mtu au taasisi.
Alisisitiza
kuwa kuna baadhi ya wagombea ambao wamekamatwa na maafisa wake na
kwamba uchunguzi unaendelea na kwamba mara utakapokamilika watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma za rushwa zinazowakabili na kwamba Ndugu Nape
sio miongoni mwao kwa sababu yeye hakukamatwa akitoa wala kupokea
rushwa.
Post a Comment