Maradhi ya Moyo kwa Watoto, Kudhibitiwa na Madaktari Bingwa Kutoka INDIA
Na Mwandishi Wetu
Kutokea
kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani
kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na
maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki. Takriban watoto 8
kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu
hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa
takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani
Afrika inaweza kuwa wengi sana.
Watoto
wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa.
baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika.
Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.

Watoto,
hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya
umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji
moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto
anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake
unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji
kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa
ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni
mgumu zaidi.
Kutokana
na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri,
Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya
Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona
kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na
mafanikio. Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu
miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto,
kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze
kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa
upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji
unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika
hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.
Wakati
mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya awali ya kuchunguza
hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya kifua na ECG
ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo (ECG)
mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa
ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu
yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika,
takwimu hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia
katheta ya moyo na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.
Uboreshaji
wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa upasuaji kwa watoto.
Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na mwongozo wa pande
tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii inatoa mpango
bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na kwa hiyo
matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.
Kuna
tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya hizi ni pamoja na
mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa kuufungua na
kuufunga.
Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na hii inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa vinavyowezesha kuipata mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii mtoto hapati maumivu ya kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona kwa haraka zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.

Namna
nyingine za matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali
mbaya zaidi ya moyo ni ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani
(upasuaji).
Upasuaji huu unaweza kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri wa masaa manne hadi matano au wenye gramu 800. Kutokana na utata wa hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi unasisitizwa zaidi. Hata mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada kutoka kwa timu.

Watu
kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi wanashiriki katika
kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Madaktari wa
watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile kudhibiti
maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia ya
kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu
zaidi kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.
Kwa
mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto Apollo,
Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza
kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito)
kupata kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika
kuchunguza moyo wa mtoto akiwa ndani tumbo la mama. Daktari bingwa wa
Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya
ujauzito. Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi
sahihi juu ya mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika
katika moyo.
Njia
nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa kuepukana ndoa
kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa, na
kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na
kasoro katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya
kuepuka ugonjwa wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa
matibabu ya maambukizi katika koo kwa wakati kwa kutumia antibiotiki.
Timu
ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai
inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto
duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya
sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii
Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro
na magonjwa ya moyo.
Baada
ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji
ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji
hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na
maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya
kwa muda mrefu maishani bila matatizo.
Inachangiwa na:
Dk Neville A.G Solomon
Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto
Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai.
Post a Comment