Taasisi ya BILL na MELINDA GATE, Kusaidia Ukusanyaji wa Takwimu za Kilimo TANZANIA
Afisa
Mwandamizi anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo kutoka Taasisi
ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates Bw. Stanley Wood akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa
kikao cha mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
nchini Tanzania kuangalia uwezekano wa taasisi hiyo kusaidia miradi ya
ukusanyaji wa Takwimu za kilimo nchini Tanzania.Kushoto kwake ni Mratibu
wa miradi wa Taasisi hiyo Bi.Bhramar Dey.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza na
waandishi wa habari Kuhusu umuhimu wa takwimu za Kilimo nchini Tanzania
na mikakati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha
upatikanaji wa Takwimu za kilimo nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw.Morrice Oyuke.
Mkuu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof.Innocent Ngalinda
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya chuo
anachokiongoza katika kutoa elimu kwa watakwimu wa kilimo nchini
Tanzania na mpango wa chuo hicho kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa
takwimu za kilimo kwa kutumia wataalam wanaozalishwa.
Mtakwimu
mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi.Elizabeth Talbert( kulia) na Meneja
wa Idara ya Viwanda na Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Joy Sawe
wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya viongozi wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wawakilishi wa Taasisi ya Kimataifa
ya Bill na Melinda Gates jijini Dar es salaam.
Picha na Veronica Kazimoto.
…………………………………………………………………………………….
Na Aron Msigwa
Taasisi
ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gate imekutana na kufanya mazungumzo na
viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)kuangalia namna ya
inavyoweza kusaidia upatikanaji wa Takwimu Bora za Kilimo nchini
Tanzania.
Akizungumza
na vyombo vya habari mara baada ya kufanyika kwa mazungumzo hayo
jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi wa Taasisi hiyo anayeshughulikia
Sera na maendeleo ya kilimo Bw. Stanley Wood amesema kuwa taasisi hiyo
imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali Barani Afrika na Tanzania ni
miongoni mwa nchi za Afrika zilizopewa kipaumbele na kunufaika na
taasisi hiyo.
Amesema
kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika
kufanikisha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo
zimekuwa na matokeo chanya, taasisi hiyo inaangalia uwezekano wa
kusaidia upatikanaji wa takwimu bora za kilimo.
”
Juhudi kubwa imefanywa na Tanzania katika kufanikisha mambo mbalimbali,
kwa upande wetu tumeona vipaumbele vilivyopo ili tuweze kuona namna
tunavyoweza kutoa mchango wetu kusaidia ukusanyaji wa takwimu Bora za
kilimo , kikubwa ni kuendelea kujenga ushirikiano wa kuwezesha ufanisi
wa tafiti mbalimbali” Amesema.
Wood
ameeleza kuwa taasisi ya Bill na Melinda Gates imekuwa ikichangia fedha
za miradi mbalimbali ya maendeleo Barani Afrika kupitia mashirika ya
kimataifa yanayohusika na utoaji wa huduma kwa umma na kuitaja Tanzania
kuwa ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika zinazonufaika na
miradi hiyo.
Amesema
taasisi ya Bill na Melinda Gate kwa kipindi kirefu imekuwa ikitoa
kipaumbele kusaidia miradi ya afya hasa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa
Ukimwi, kusaidia huduma za Afya ya mama na mtoto pamoja na kuweka
mkazo katika kuimarisha huduma za maji safi na maji Taka Barani Afrika.
Post a Comment